(TOTAL INDEMNITY)

MALIPIZI TIMILIFU.

April 3, 1983-KOREA

 

Leo, niacheni niongee kuhusu malipizi timilifu. Malipizi timilifu inahusisha dini, historia, pia jamii ya binadamu kwa ujumla. Inahusisha sio dunia ya kimwili peke yake, hata dunia ya kiroho vilevile.

Nia asilia ya Mungu kwa Dunia ilikuwa nyepesi. Yeye aliwazia dunia moja ambayo ingekamilika endapo Adamu, Eva, Mungu na Dunia ya Malaika wangeungana kuwa moja kabisa. Nia ilitoka kwa Mungu na ilitakiwa kupitishwa kwa mababu wetu wa kwanza kama Wazazi wa kweli wa watu wote. Kuanzia na sehemu ile ya asili, nia ingepanuka kimlalo kwa dunia nzima, kwa kufanya dunia ilioungana kabisa.

Katikati ya kila kitu kuna upendoo wa Mungu. Mungu anahitaji upendo, mtu anahitaji upendo, na wamalaika pia wanahitaji upendo. Ikiwa dunia ilitawaliwa na upendo wa Mungu toka mwanzo, ingekuwa sio mwanzo mzuri tu, lakini mwelekeo na matokeo ya mwisho pia yangekuwa mazuri. Mungu; mtu na wamalaika wangeumba dunia moja kamilifu, kwa kushirikiana kwa uhuru chini ya upendo wa Mungu.

Bais, mtu anakua mkamilifu sio kwa kuwa tajiri au kwa kupata nguvu na ufahamu kidunia, lakini kwa upendo huu sio upendo wa kidunia jinsi ilivyo katika dunia ya anguko, lakini upendo asilia; Kila kitu kimetimilizwa na kukamilishwa kwa upendo huo;

Tuna milango mitano ya maarifa ambayo inatuwezesha kuona, kusikia, kunusa, kutomasa (papasa, gusa) na kuonja dhuku. Zile zingetumika chini ya upendo kamilifu, pia macho, masikio, pua, mikono ya maarifa chini ya upendo ni hali nzuri/bora sana. Ni kama hali ya kupotewa akili, lakini kwa upendo. Mnajisikia mrushwa akili na mazingira, kwa kupata uhusiano wa kubadilishana na kila kiumbe kingine. Mmoja hawezi kamwe kujisikia akiwa peke yake; Kila kiumbe kinafikia milele, na kila kiumbe kinajifahamisha kwa njia ya pekee; Uzuri mkubwa wa dunia kamilifu ungepatikana kwa njia ya uhusiano mkubwa mbali wa kubadilishana zilizoendelezwa baina ya vitu vyote vya uumbaji.

Nguvu za upendo wa kweli inaweza kutambaa bila mwisho, na wakati huo huo inaweza kubanwa katika doa dogo mno kabisa. Hii ni sheria ya kimbingu. Kwa hivyo, tukiangalia kwa macho ya upendo, kila kitu kina thamani. Ndani ya kitu kidogo thamani imebanwa, na ndani ya kitu kikubwa imetanuka. Mungu na nafsi ya kuongoza kila kitu kwa kufanya upendo kiini cha vitu vyote. Upendo ni mtiririko ambaye kwa njia yake Mungu anaweza kutawala juu ya ulimwengu kupita muda na mahali. Bais, kwa kutawala juu ya ulimwengu, Mungu mwenyewe anahitaji kabisa upendo huu; Kwa kufikiri kinamna hii, tunaweza kuona kwamba hakuna hata kiumbe kimoja kina thamani bila upendo wa kweli.

Kusudi la Mungu lilipotezwa na anguko. Walimwengu walianguka vipi? Kwa njia ya upendo. Mahali pa mwanzo wa upendo sio jicho wala mdomo, lakini ni viungo vya uzazi vya mme na mke. Mahali pa muunganisho wa upendo ni mahali ambapo fadhaa zote zinakuja pamoja/zinajumlishwa kipeo cha kweli cha upendo kilipotea mahali hapo, kwa hivyo uhusiano wa mme na mke ulikua chanzo cha matatizo yote ya ulimwengu mzima.

Kwa sababu hii, ilibidi kila kitu kinakombolewa au kinaumbwa (upya) tena. Hii tutakifanyaje? Tukio kubwa moja la anguko ni kwamba tukaja chini ya mabawa mawili, au watenda wawili. Kama tulikuwa na mtenda mmoja au bwana mmoja, isingekuwa tatizo kubwa hivyo kukomboa kila kitu halafu kurudi katika hali asilia. Kama Mungu angekuwa bado mtenda mmoja peke yake, kila kiumbe kingelingana na yeye pia kusingekuwa na chocote cha kupinga ulinganifu huu. Lakini kuna mtenda mwingine, ambaye mwelekeo wake ni kinyume kabisa na ule wa Mungu. Kiumbe kile kilichukua na nafsi ya mtenda kwa kumkana Mungu. Kama tukio moja la anguko, nguvu za kupinga za upendo ambayo inamvuta mtu mbali sana na Mungu ikawa hodari zaidi kuliko nguvu inaomuongoza mtu kurudi katika chanzo chake asilia. Hivi hivyo, nguvu ya upendo ikaja kutenganishwa (kugawanywa) katika kambi/pande zinazopingana za ndani na nje. Shetani amefungamana na dunia ya upendo chini ya nguvu ya nje/kimwili, halafu Mungu amefunganwa na upendo chini ya nguvu ya ndani/kiroho. Kwa hivyo, watenda wawili wakaja kusimama juu ya mtenda mmoja, mtu. Shetani akawa mtenda wa kimwili/nje, wakati Mungu akawa mtenda wa kiroho/ndani.

Kila mmoja wao yuko katika nafasi ya chanya-kiroho au kimwili-kwa hivyo, wanafukuzana/wanarudishana nyuma. Hii imedhihirishwa ndani ya shindano kati ya mahitaji ya kimwili na dhamiri ya mtu alieanguka. Wanatakiwa kuwa mmoja lakini wanafukuzana, wanazuiana. Mtu anavutwa katika maelekeo mawili tofauti vile kama alikuwa na maumbile mawili yanaofukuzana. Kwa hivyo, mtu alikuwa kiumbe kilichopoteza mwelekeo. Wakati mmoja anaenda upande wa nje na wakati wengine upande wa ndani. Kwa kuwa mtu anageukageuka kila kitu kandokando zake kimeambukizwa. Adam na Eva wakawa mme na mke wa aina hiyo. Kama kuna watu 10, wana maelekeo 10 tofauti; wametawanyika. Dunia ilikuwa dunia moja ya chafuko kama tokeo la anguko.

SABABU AMBAPO SHETANI ANATAKIWA KUKATALIWA

Dunia la nia asilia la Mungu iko wapi? Yatupasa kutafuta nia asilia na kutenganisha tena dunia la anguko. Hii sio rahisi. Kwa kukifanya, yampasa Adam kujikana mwenyewe na yampasa Eva kujikana mwenyewe. Kama kunajmaa 10 ndani ya familia moja, na wote 10 wanajaribu kufanya umoja kwa kujidai wenyewe, umoja ni muhali. Kama kuna wanajamaa 10 ndani ya familia moja, wote 10 wanatakiwa kujikana wenyewe. Kabla ya kitu kingine chote, Mungu hana budi kuomba kujikana mwenyewe katika dunia ya anguko la watu. Kabla ya kutafuta kusudi, yeye hana budi kutafuta mkano, mkano wa anguko. Mtu hana msingi wowote wa kujdai. Hii ni mtazamo wa Mungu.

Halafu nini kanuni/taratibu za mkano kama huo? Ni toka nje kwenda ndani. Katika mtiririko wa anguko, kuna dunia ya nje ya taifa, jadi, na ukoo, sawasawa na familia. Tena kuna kiungo-mme na mke pamoja. Hatuna budi kujikana wenyewe kuanzia nje, toka upande wa nje. Mwisho, mahali tunapofikia ni mkano wa mwili wetu na mawazo yetu. Inatubidi kwenda umbali huo. Tunaishi kati ya dunia ya anguko, hivi kwa kutafuta matakwa ya Mungu, kutafuta mahali pa kujidai nchini, hatuna budi kukana dunia ya anguko kabisa. Mahali mpya pa kuanzia inaanza tu baada ya kukamilisha kipeo hicho. Hili ni neno la uhakika. Kwa sababu gani tunahitaji malipizi yaliyofundishwa na Shirika la Umoja? Yatupasa kujua sababu wazi. Si hata moja baina/baadhi yenu anaelewa wazi maana halisi ya malipizi kwa mtu peke yake, malipizi kwa familia, ukoo, jadi, na malipizi kwa taifa. Kwa sababu gani tunafanya kitu kama hicho? Hii ni jambo la maana sana.

Kwa Mungu kufanya mwanzo mpya, lazima yeye asafishe kila kitu. Sharti asiwepo kiumbe kingine kama mtenda, shetani asiwepo. Lazima Mungu awe mtenda kwa uhakika na peke yake. Mungu hawezi kukaza (kuweka) mahali pake pa kuanzia upya bila nafasi ya shetani kung'olewa kabisa. Kwa mtu kujikana yeye mwenyewe sio tatizo moja kubwa. Tatizo ni kumkana/kumkataa shetani ambaye anatawaliwa/anaongoza mtu. Basi, baada ya mtu kujikana mwenyewe kabisa, Mungu hana budi kuweka kanuni kumkataa kabisa. Kama sivyo kutabaki bado watenda wawili. Hata mtu akijikana mwenyewe, Shetani atabaki bado. Kama mtenda geni ambaye anaongozwa na upendo batili, anasidia/anabaki hadhara ya Mungu na ulimwengu, kuna kanuni mbili, na hatua ya mwanzo ya utimilifu haiwezi kufanyizwa. Tutawezaje kumkataa shetani? Hii ni sharti ya lazima kabisa kwa ajili ya kufanya mahali pa kuanzia upya nchini/duniani kwa Mungu na walimwengu. Yatupasa kuona kukataliwa kwa Mungu batili. Mungu mwenyewe anaweza kusimama kama mtenda endapo tu yeye atasimama juu ya msingi wa huo wa mkano pia anakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi yake ya mtenda wa upendo. Je mnaelewa?

SHARTI LA UKANI KAMILI

Basi, sharti hii inafanyizwaje? Anguko lilianza na mtu mmoja, Adam. Kwa kuwa mtu peke yake ni kiini cha jamii yote, ili kuikomboa dunia hii(dunia) ilianguka, hatuna budi kusonga mbele hatua kwa hatua; haiwezi kufanywa kwa mara moja. Tatizo la dhambi lilipanuka kupitia daraja nane: toka mtu peke yake, familia, ukoo, jadi (au watu), taifa, dunia, ulimwengu, na Mungu. Mtu, ambaye anatafuta dunia kamilifu, hawezi kupata njia yake ya kumrudia Mungu, ambaye ni mtenda asilia wa upendo, asipo shinda matatizo haya. Kama daraja moja itafikiliwa, mtu anaotawala chini ya daraja hilo, lakini yeye hawezi kufikia dunia kamilifu kushinda/mbele ya kiwango hicho au kuungana kabisa na Mungu mkamilifu. Mtu mmoja anapofikia daraja fulani, watu katika ulimwengu wa kiroho ambaye walishafikia kiwango sawasawa cha ukuaji wanaweza kumsaidia, na anaweza kushirikiana nao; walakini, ni vigumu kwake kushirikiana na Mungu asilia. Mazingira yatawezaje kutanuka ili mtu aweze kushirikiana na Mungu? Jambo hili ni wasiwasi wa Mungu mwenyewe, pamoja ni shaka la mtu ambaye yuko katika mtiririko wa anguko. Mashaka haya mawili yameongezekewsa ugumu na mtu wa dhambi yeye mwenyewe. Mtu alieanguka anatawaliwa na malaika mkuu; hakuna kabisa uwezekano wa kubadilisha utaratibu huu wa thibitisho ila kwa ukani. Halafu, ukombozi kwa njia ya malipizi ni nini, yule anaetaka kufikia mtenda mmoja timilifu lazima akamilishe sharti la ukani yakinifu katika uhusiano na kila kitu katika mazingira yake. Kwa hii, ukani yakinifu unatakiwa. Basi, na nafasi gani ukombozi kwa njia ya malipizi unakuwa umekamilika? Hata ka-kipande kadogo ka sharti la kujiyakinisha yasiweze kubaki. Lazima iwe kabisa katika mtiririko wa ukani. Sharti la malipizi imelipiwa kwa kukamilisha sharti la ukani yakinifu. Kipeo hicho kinapokamilika katika daraja zote nane, toka mtu peke yake, familia, ukoo na kadhalika, mtu anaweza kufikia dunia timilifu wakati wa utimizo wa historia ya binadamu. Mnapaswa kwa lazima kwenda kwa njia ya utaratibu katika kila moja ya daraja hizo nane. Kama sivyo, hakuna atakae fikia ukamilifu ambapo ataweza kushirikiana na Mungu.

Mungu anafumbua ukweli wa dunia ya anguko, kwa kujaribisha/kutunga kwanza kifani kimoja, kuliko kujitahidi kukomboa jamii yote. Kwa kuzalisha tena na kiwango kikubwa, tunatangulia kutunga kielelezo (kiolezo). Na kiwango cha mtu peke yake, tunatunga kielelezo kwa mtu mmoja. Halafu tungehitaji kutunga kielelezo cha familia kwa kiwango cha familia. Toka ukoo, jamii, hadi taifa, hatuna budi kufikiri hivi hivi. Kulingana na kanuni za uumbaji, inatubidi kupitia hatua tatu ya mwanzo, kukua na ukamilisho katika historia ya binadamu kwa ajili ya kutunga kielelezo kwa mtu mmoja. Yatubidi kutunga mazingira na kufanyiza kipeo cha kubadilishana cha upendo. Kiini cha mtiririko huo wa kubadilishana ni mtu, na kiini cha mtu ni upendo. Yampasa mtu kujilipizia mwenyewe na kiwango cha mtu peke yake. Kufanyiza kipeo kwa mtu mmoja sio rahisi.

Kwa kupitia historia nzima hadi leo, kwa sababu gani wanawake waliwekwa mbali na ushirika kamili katika dunia ya mambo ya Mungu? Hata hivyo, maongozi ya Mungu wa upendo yaliendeshwa kwa uongozi wa wanaume, na wanawake waliwekwa mbali sana. Kwa nini ilikuwa hivyo? Kwa kutunga mfano wa mtu mkamilifu, kielelezo cha uumbaji kilikuwa hivi: kwanza Adam aliumbwa, na baadaye Eva. Hii ilikuwa kielelezo. Lakini, kifani kwa ukamilifu sio nzima kwa mtu peke yake. Ulimwengu wa malaika ulishiriki na Mungu katika kuumba kielelezo asilia cha mtu, chini ya uongozi wa roho. Kwa hivyo, Mungu ndiye kiini cha roho pia kiini cha dunia ya kiroho. Mtu anaweza kusimama na nafasi ya kifani endapo tu anaweza kuyeyusha ulimwengu mzima wa vitu vyote na kumezwa kabisa pamoja na Mungu.

Msimamo wa maisha kwa mtu wa dini kweli ni ule ambao amemezwa kabisa. Ni utii kamili; kwa hivyo, hawezi kudai nia yake au kauli yake juu ya yale ni ya Mungu. Lazima yeye afuate kabisa nia ya Mungu. Ni mazingira ya kujihini kabisa, lakini tena yambidi kumezwa kabisa na Mungu. Kama mtu atadai unafsi wake yeye anachukua nafasi ya chanya mbele za Mungu, ambayo inamfukuza/inamchukiza Mungu. Hii inamwacha mtu ndani ya mazingira ya mtenda anaempinga Mungu, ndiye Shetani. Hii ina maana kwamba yeye anakuwa miliki ya Shetani. Vile vile, yeye hawezi kamwe kufikia ulimwengu kamilifu wa Mungu. Na nafasi hii katika ulimwengu wa dini, utii yakinifu unahitajika Waumini toka Ulaya kuelewa jambo hili wazi. Kwa sababu gani utii unahitajika? Kufuata mawazo yanu binafsi inawaongoza kusimama na nafasi ya kuwa na mtenda wa pili. Mtenda wa pili ni Shetani, kwa hiyo mnakuwa mtendewa wa Shetani. Mkinenea kwa nguvu juu ya mawazo yenu binafsi kuwa msingi wenu, unaweka sharti kwa Shetani kutawala juu yenu. Mungu na Shetani wamo katika kambi mbili zinazopingana, wakishindana kwa kutawala juu ya dunia binadamu walikoanguka. Kusudi asilia ya kuwako kwa binadamu vile vile na kusudi asilia ya Malaika mkuu ni kwa ajili ya ukamilifu wa lengo. Hii Shetani anafahamu pia.

ULIMWENGU WA UKANI KWA NJIA YA UDHALIMU

Kiasili Mungu alituumba na kusudi la ukamilfu kuwa lengo lake. Shetani anajua hili pia halikatai. Kufanyiza sharti kamili ambalo litatuwezesha kufikia kusudi la ukamilifu sio rahisi. Inahitaji hali ya kujihini kikamilifu. Hatuwezi kufanya hivi kama tutanena kwa nguvu juu ya mtazamo wetu.

Tukiangalia dunia, wapi tunaweza kupata /kukuta hali ya kujihini? Ni vigumu kuikuta katika tabia ya upande wa magharibi, ambayo inaainisha upendo wa uhuru. Tukio la mwisho la uhuru kama huo ni kwamba kinachobaki ni nafsi peke yake. Waume na wake wanaishi pamoja, lakini kila moja wanadai njia zao. Kwa hali hiyo, kuna madai mawili ya uhuru. Kama kuna watu wanne pamoja, wanadai manne ya kila mmoja. Kama kuna watu 10, kuna madai ya watu 10 kwa uhuru wao. Mwisho, wanaenda kila mtu njia yake na wote wanatengwa na kutawanyika. Hakutakuwepo umoja ndani ya familia au mataifa. Ingawa mtu (mmoja) anashindana kufurahiwa na tabia yake asilia kwa njia ya uhuru, kwa kweli anapoteza kila kitu na (anaanguka) anaporomoka katika vilindii vya kufa moyo. Anapogundua kuwa hawezi kuridhisha matamanio na malengo yake binafsi, analenga juu yake. Hii ni ukweli kwa wengi katika ulimwengu huru leo, sana sana America. Lakini kufa moyo sio sehemu ya matakwa ya Mungu. Katika dunia kama hii, hakuna kanuni ya ukamilifu ambayo Mungu anataka. Kwa sababu hii, mawazo ya upande wa Mashariki, zaidi ya yale ya upande wa Magharibi, yanatoa uwezo kwa Mungu. Ndani ya fikira ya upande wa Mashariki, kuna kanuni ya utumishi kamilifu kwa wazazi, na kwa wakati huo huo wazo la kufuata makaka na madada wa kubwa. Wakati wazo hili la utumishi litapanuka, linaweza kufikia kiongozi wa ukoo, kiongozi wa jamii, au wakili/mwakilishi wa taifa. Kwa hivyo tunaweza kunufaika na msingi kwa kutegemea shauri kamilifu la utumishi. Isivyo, hatuwezi kamwe kuwa na familia, ukoo, jamii, taifa, au dunia ambazo Mungu anataka. Lazima mwelewe hii wazi. Basi Mungu ataumbaje mazingira ya aina hii? Yeye hawezi kukifanya kwa kusema, "Nyie watu wa dini yawapasa kukamilisha kujihini kwa nguvu zenu wenyewe!" Hapana, hatuwezi kufanya hivyo kwa njia ile. Kipeo cha kujihini lazima kikamilike ndani ya uhusiano mbalimbali wa kubadilishana. Kama mmesukumwa katika nafasi ya kukataliwa na mtu mwingine, ni sawa sawa na kujihini mwenyewe anaefanya. Kwa hivyo, mtu wa dini atapingwa na watu wote. Hii ndio maana kabisa ya udhalimu. Wakati mmoja anaamini Mungu pia dini, mara nyingi wale ambao wako karibu sana na yeye vile kama wazazi wake au wapendwa wake, watampinga. Katika hali kama hiyo, Shetani, kama mtenda wa pili, anakuwa akimshambulia mtenda wa kwanza, Mungu. Mtu mwenye haki anapopigwa na mtu mwingine kwa jeuri(udhalimu), tendo hili linaweka sharti ambalo lazima lilipwe. Kwa sababu ya kulipa hii, maendeleo ya dini yanakuwa yamewekwa salama. Je mnaelewa kwa sababu gani udhalimu unatokea?

Ndani ya mtiririko wa dini, Mungu yampasa kupanua desturi ya kujihini toka kiwango cha mtu peke yake hadi familia, ukoo, jamii, taifa, na dunia. Watu hawawezi kujifanyia hivi wao wenyewe. Kati ya ukombozi kwa njia ya malipizi, mtu anaelekea kuwaza kwamba kipeo cha kujihini kwa mtu peke yake kinatosha, lakini sio kweli. Kipeo cha malipizi ya mtu peke yake kinapaswa kuelekezwa upande wa malipizii na kiwango cha dunia, ule msingi wa kujihini lazima utungwe. Binadamu mwenyewe hakugundua jambo hili, lakini Mungu na Shetani wanalifahamu. Watu hawajui kanuni kamili ya kuani; kwa sababu hiyo, Shetani, ambaye anaielewa, anashambulia mtu kwa kumkataza ukani wowote wa mtu mmoja ambao unaelekezwa upande wa kiwango cha dunia. Dunia ziliendelezwa katika kipito cha historia hadi sasa sawasawa kwa sababu zilijiendekeza kujihini na zilipokea udhalimu. Hii ilikuwa hivyo, ingawa hakuna hata mtu mmoja aliejua kwa sababu gani. Sasa ninawaambieni sababu. Kwa kuwa mtu hawezi kutenda kujihini akiwa peke yake, badala ya hapo, Mungu anamruhusu Shetani mwenyewe kumkana mtu. Na kama mtu ataibuka na ushindi katika mtiririko wa ukani, basi yeye anaweza kudai ushindi juu ya shetani. Yeye anaweza kumilikiwa na mtenda wa kweli, kwa jina (ni) Mungu. Kama tukio la udhalimu, au kujihini yakinifu mbele ya uso wa Mungu, mtu anaweza kuingia katika ulimwengu wa ushirikiano/uhusiano wa kubadilishana na Mungu. Hivyo, Mungu anaweza kumwingilia kati. Hii ndio sababu dini iliendelea zaidi kwa njia ya udhalimu.

Kwa sababu hii, mtu hawezi kupata ukamilifu wa aina ya dini kwa kuacha dunia hii na kwenda juu ya milima kwa kutafakari. Mtu anaweza kufikia ukamilifu hivi hivi tu kwa kusimama katikati ya dunia na kupokea udhalimu wote toka kwa Shetani. Lakini ili kufikia umoja na Mungu, mtu anatakiwa kishinda mashambulio ya Shetani. Yeye hawezi kulemezwa kati ya udhalimu. Kwa hiyo, Mungu alijaribu kufanya kazi kwa njia ya watu wengi katika historia lakini ilimbidi kuwa acha mwishoni. Mungu aliweza kutumia baadhi ya watu katika maongozi yake kwa muda wa miaka kumi au hata karne. Bado mwisho wake, iliwabidi kusimama katika mtiririko wa udhalimu, ushindi wa mtu mmoja unaweza kubaki. Lakini kama yeye hawezi kupitia mtiririko wa udhalimu wa kifamilia, yeye ataangamizwa. Kwa hali hiyo, Mungu lazima ampate mtu mwingine ambaye ataendelea naye kati ya maongozi yake. Kama mtu mmoja amelemaza, hakuna chochote Mungu anaweza kumfanyia. Mungu analazimishwa kumtafuta mtu mwingine; hii ilikuwa njia ya mashaka ya historia ya dini hadi sasa. Kwa kuelewa mambo haya ya kawaida, mnaweza pia kuelewa jinsi gani kuendelea mbele na ukombozi kwa njia ya malipizi. Hamwezi kujihini wenyewe mkiwa peke yenu. Basi, lazima mstahimili/mvumilie sharti la ukani kwa njia ya udhalimu. Kwa hiyo, udhalimu una haja kabisa katika maongozi ya Mungu ya dini na hakuna njia ya kurudi kwa Mungu bila kupitia njia hiyo ya udhalimu. Hakuna hitilafu kwa amri hii. Dini zote za dunia, vile kama Ukristo, buddhism, confucianism, zote zilipita njia ya aina hii. Hii ndiyo sababu zinasimama na kiwango cha maendeleo kidunia. Dini zenyewe hazikulewa sababu hii hadi sasa. Hazikuweza kueleza sababu za watu wa dini kulazimishwa kupitia njia ya mateso/tabu na udhalimu, lakini sasa nyie mmeelewa jambo hili. Ni mwisho wa uhakika kwamba ukamilifu timilifu ambao ninazungumzia haufanyizwi bila malipizi timilifu. Kwa kuongoza kila kitu katika mtiririko wa ukamilifu, lazima tupitie utaratibu wa malipizi timilifu. Hili ni jambo la muhimu kabisa katika historia ya dini. Kwa hivyo, ni vibaya kufikiri kwamba mtu atakuwa na maisha (ya starehe/rahisi) kwa kufuata dini.

NI NANI MASIHI?

Ndani ya Ukristo, kuna imani katika Ujio wa Pili wa Masihi. Ni nani Masihi? Masihi ni yule ambaye Mungu anampenda zaidi. Ni nafasi gani ambayo inapendwa zaidi na Mungu? Kuna watu wengi ambao wanasimama mbele za Mungu kama wawakilishi, kwa mfano, wa taifa, jamii, au shirika nyingine fulani. Masihi ni mtu wa aina gani? Masihi ni mtu wa kwanza ambaye ana moyo wa upendo pia mwelekeo wa upendo sawa sawa na Mungu. Masihi ni mwanaume kifungua mimba wa Mungu. Yesu alikuwa mtoto mume wa pekee wa Mungu, mtoto wake wa pekee. Kuwa mtoto wa pekee ina maanisha kupokea upendo wote wa mzazi, toka mwanzo hadi mwisho. Mungu ni mtenda mtimilfu na Masihi anasimama katika ulimwengu wa Mungu. Uhusiano wao ni uhusiano wa mzazi na mtoto. Yeye ni yule ambaye amezaliwa kama mtoto mume wa kwanza na anapokea upendo timilifu wa Mungu anaopewa namtu, familia, ukoo, jamii, taifa na dunia. Yeye anastahili kupokea upendo unaozidi sehemu hizo zote. Huyu ndie Masihi. Yeye ni mtoto mpendwa wa Mungu.

Lakini kipi anaweza kukifanya kwa uwezo wake pekee? Mpendwa anatakiwa kupata mke/mchumba wake, na anaweza kumpata wapi? Yeye hawezi kumpata akitoka Mbinguni. Kwakuwa mwanadamu alipotezwa kama tukio la anguko duniani, yeye analazimika kuumbwa tena duniani. Dini nzima itafanya nini? Mbinguni iko katika nafasi ya chanya na nchi iko katika nafasi ya hasi. Watu wanataka Masihi, ambaye anajua Mbingu. Dunia hii ya watu inataka sana mtenda wake halisi wa upendo na uchu huu ni uchu wa Masihi. Masihi anatakiwa kupokelewa na kiwango cha dunia, kuzidi kiwango cha mtu, ukoo na hata taifa. Dunia nzima itakuwa na uwezo wa kuungana na mtu mmoja wa upendo wa Mungu, kama mtenda yakinifu. Hakuta kuwa na sababu ya kumpinga; kutakuwepo tu utumishi yakinifu. Unafiki hauwezi kuwepo tena. Kuunda mazingira ili mtu aweze kuishi tu kwa ajili ya Bwana ilikuwa kazi ya wakati wa Agano la kale na wakati wa Agano Jipya. Kazi ya nyakati hizi zote mbili ilikuwa pia kuumba Eva mmoja, mke mmoja, kwa ajili ya Masihi. Mara moja tu Eva anamfuata Masihi kabisa na mtiririko wa utii imepanuka, uzio Masihi utapungua. Katika mazingira haya, dunia nzima itafungishwa moja kwa moja na mtenda wa upendo na nafasi moja. Kutunga mazingira kama vile na kiwango cha dunia ndiyo ilikuwa kazi ya wakati wa Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa hiyo, Ukristo na Uyahudi wa siku ya leo wanatakiwa kabisa kumfuata Masihi. Wakristo na Ayahudi ambao walikuwa wakitunza imani yao (wanadhaniwa) wanahitaji kutoa kila kitu ajapo Masihi. Imani yao inafundisha utii yakinifu kwa Masihi. Lakini ukweli wa Wakristo wa siku ya leo ni nini? Nini kuhusu Wayahudi leo? Badala ya roho ambayo Mungu anaitaka, wao wamekuwa wanapinga kabisa, manyuzi 180. Kama dini moja inataka tu ustawi wake pekee duniani, na inadharau Masihi anaerudi na inazuia kumalizika kwa ushindi kwa maongozi ya Mungu, ile dini itakuwa legevu kabisa katika siku za mwisho, vile kama ilipigwa na nyundo ya Kimbingu ya Mungu.

Katika kipindi hiki cha siku za mwisho, Wakristo duniani wanatafuta Bwana wa Ujio wa Pili, lakini kama tutachunguza maana,sababu ya msukumo wa uchu wao, inakuwa kwa kawaida, "Mimi nataka kuokoka". Hakuna shaka kwa ushindi wa Mungu na kiwango cha dunia. Wanaweza kusema,"Mimi nataka kuokoka." Kadiri ya mwisho ni kwa kawaida nchi. Lakini lazima waende zaidi ya nchi hadi mwisho wa dunia; lazima wapanue shaka zao hadi dunia ya kiroho. Lakini zaidi yao hawawezi kwenda zaidi ya nafsi zao wenyewe na hii ni ushindi kwa Shetani. Kwa kipeo hiki kitabaki, dunia ya Mungu haiwezi kuzaliwa.

SHIRIKA LA UMOJA NI NINI?

Sasa hatuna budi kuanzisha kundi moja jipya duniani ambalo linagawa dunia katika pande mbili. Hatuna budi kukamilisha kusudi la Mungu la utimilifu wa dunia na kulitanua kwa ulimwengu wote. Kama kundi la kidini lenye kusudi kama hili halitatokea, maongozi ya Mungu hayawezi kukamilika. Itakuwa sawa na kama Mungu hayupo. Kwa hivyo, kama Mungu yupo na kama yeye anajaribu kukamilisha kusudi lake, kundi kama hili lazima liundwe duniani. Hoja hii ni ya uhakika. Ni kundi gani hili? Kwa kweli ni Shirika la Umoja. Shirika la Umoja linalazimika kuwa na madhumuni pia msukumo ndiyo hasa niliyosemea. Kwanza kabisa lipaswa kukuza kujihini toka kiwango cha mtu mmoja hadi kiwango cha dunia. Ajapo Masihi, kama Ukristo utamfuata kabisa na kuungana naye kabisa, utakuwa umekamilisha kusudi lako. Ajapo Masihi na kujitangaza, hapo kila mtu atalazimika kuungana naye. Lakini hawawezi kufanya hivyo hadi atakapo kuja. Kwa sababu hiyo, Mungu alikuwa anaongeza urefu wa maongozi yake katika historia ya anguko la mamia ya maelfu ya miaka hadi sasa.

Mungu yupo, walakini kadhalika udhalimu upo. Kwa sababu gani Mungu aliacha Wakristo wa kwanza wateseke kwa miaka 400 katika Urumi wa zamani? Kwa kukagua kanuni, tunajua kwamba udhalimu uliendelea mpaka kipeo kilichoweza kufaa kote duniani kilionekana. Kwa hivyo, Ukristo ulifikia kiwango hicho baada ya miaka 400. Juu ya msingi uliowekwa na Ukristo, Kanisa la Umoja lilitokea duniani baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia. Ukristo hauna budi kusikiliza neno la Masihi linalotazamiwa toka mtazamo kamili wa maongozi ya Mungu. Kwa vyo vyote wakimsikiliza au sio inakuwa jambo la uhai au kifo kwa Wakristo. Kama mtu anaamini maneno ya Masihi, yeye anaweza kupata uokovu kiroho; kwa sababu hii, yampasa kujikana yeye mwenyewe. Mtu yampasa kuweza kukana kila kitu; historia yake ya zamani, familia yake na hata upeo wake wa imani wa zamani. Kama yeye ataweza kuona kwamba Masihi ndiye mtu ambaye alikuwa anamtafuta, jisni anavyoonekana kwa miwani ya historia kibiblia, hakuna tatizo lolote. Lakini kwa wengi, miwani yao haifai. Wanaangalia vitu kwa miwani ya ubinafsi wao, kwa sababu hiyo hawamtambui Masihi wanapomuona. Masihi anakuja na kiwango cha ulimwengu; kwa hivyo mtu asimpime/asimkadirie kwa kipimo chake binafsi. Kama mtamsikiliza au kumuona kwa mtazamo wenu binafsi tu, hamtaelewa yaliyomo ya ujumbe wake. Masihi anajihusisha na vitu na kiwango cha milele, kwa kujadili mambo ya labda miaka 20 au 30 ijayo.

Kama mtazamo finyo utazidi miongoni mwa Wakristo, ajapo Bwana wa Ujio wa Pili, watampinga. Kama watampinga, wataporomoka moja kwa moja ndani ya ulimwengu wa Shetani. Masihi ni yule aliyezaliwa kama asili ya upendo wa milele wa Mungu katika randa hili linaloitwa dunia. Yule anaeongoza upinzani kwa Mungu ni shetani. Yeyote atakae chukua nafasi nyingine ya mtenda, kwa jina kwa kumpinga Masihi, atakuwa sehemu moja ya ulimwengu wa Shetani moja kwa moja. Ingawa kutaweza kuwepo idadi kubwa ya watu kule, bado ni ulimwengu wa Shetani. Wale waliotakiwa kujenga msingi wa kukubaliwa kwa Masihi, kinyume na hapo, walimgeuzia bunduki zao na sasa wanasimama upande wa mbele wa jeshi/kikosi cha Shetani. Wamefikia kumkana Masihi mwenyewe. Mara tu baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ulimwengu wa utamaduni wa Kikristo duniani, kwa kuongozwa na America, ulinufaika na nguvu zake kubwa zaidi. Kulikuwa na wakati mmoja tu ambapo dunia ilienda kabisa upande wa mtiririko wa dini; ile ilikuwa muda kabisa baada ya Vita Kuu ya Pili ya dunia. Sehemu ndogo tu ilienda upande wa wasovieti, wakati sehemu iliyobaki ya dunia ilikuwa sehemu ya ulimwengu wa Kidemokrasia, mtiririko wa utamaduni wa Kikristo, ulioongozwa kabisa na America. Ikiwa America yenyewe, ambayo ilikuwa mtenda(kiongozi) wa nchi nyingine za dunia, ilimfwata kabisa Masihi, nini kilichojilia dunia? Dunia ingegeuka kwa urahisi kuwa dunia ya Mungu. Lakini nini kingetokea ikiwa mambo hayangetokea hivyo? Dunia ingerudi tena katika ulimwengu wa Shetani na kama tukio lake wangefanya shambulizi kabisa kwa kukabiliana na mkuu wa maongozi ya Mungu.

UTIMILIFU WA UKOMBOZI KWA NJIA YA MALIPIZI

Kwa mtazamo wa mbingu, nini kazi yangu? Nilipokea udhalimu usio na mwisho toka kiwango cha mtu peke yake hadi kile cha familia, ukoo, jamii, taifa, dunia, na ulimwengu. Hakuja wahi kuwepo kitu kama hiki katika historia. Ninani ambaye alipokea udhalimu mkali na mkubwa zaidi katika historia ya dini? Jibu lenu sio kwa sababu ya nyie kuwa washirika wa Kanisa la Umoja; hata wale ambao sio Washirika wa Kanisa la Umoja wanajibu kwamba ni Reverend Moon. Watu waliopo madarakani Amerikani kwa uhakika wangejibu hivi hivyo. Hata wa communisti wangejibu hivyo hivyo. Tukiwauliza watu wa imani ya Kibuddha, Wakristo, au mtu yeyote wa dini,"katika historia ya viongozi wa dini, nani aliedhulumiwa zaidi katika maisha yake, toka kiwango cha mtu peke yake hadi kiwango cha dunia?" Watajibu kwa uhakika kwamba ni Revereland Moon. Itaendelea hivi kwa miaka mingapi? Miaka sitini? Nitaenda njia ya malipizi kwa namna pungufu kwa miaka 40.

Mungu yuko katika harakati ya kutafuta mtu mmoja ambaye anaongea ukweli kuhusu Shetani, dunia, na Mungu, sio kwa ajili yake binafsi lakini ni kwa ajili ya dunia na Mungu, mtu ambaye anaweza kuchukua jukumu kwa kuongoza dunia na kwa kufundisha njia ya kujitoa mhanga. Kama kuna mtu kama huyo, lazima kwa uhakika achukue jukumu kwa njia ya maongozi ya Mungu pia njia ya malipizi. Hatuwezi kuongea kuhusu ukamilifu wa mtu peke yake bila ukamilifu wa malipizi, kwa kuwa ukamilifu wa mtu hauwezi kufanyika katika mtiririko wa Shetani. Mara moja tu tunaweza kukamilisha hii, ni mwisho wa dunia ya Shetani. Katika wazo la ukamilifu, ukamilifu wa malipizi unahusika moja kwa moja. Ukamilifu wa mtu mmoja lazima uhusishe ukamilifu wa malipizi. Hakuna hata mtu mmoja katika dunia hii ya anguko anaeweza kutimiza ukamilifu wa nafsi. Kwa mtazamo wa Mungu, ukamilisho wa malipizi ndio ukamilisho wa ukombozi, kwa hiyo, ukombozi unakamilika kwa njia ya malipizi. Basi, malipizi inakuwa neno liongezalo maana kwa ukombozi na kadhalika kwa kuridhika. Mtu asiyefurahia ukombozi kwa njia ya malipizi ni ufalme wa mashetani hata yeye akiwa mshirika wa Kanisa la Umoja. Na nyie je? Kwa kuwa mlikuwa mnapita njia ya ukombozi pamoja na mimi mliweza kusema, "Loo Baba, tulipitia njia ya ukombozi kwa malipizi, na ukombozi zaidi kwa malipizi. Itabidi kuendelea tena miaka mingapi? Iliendelea hivyo miaka 10, na tena miaka 20 mingine!" Hilo ni kweli. Kala hatutafanikiwa kuingia ndani ya mtiririko wa ukamilifu kwa mara moja, kipitio chetu chenyewe kinaongezeka urefu mara tatu(zaidi). Hilo ndilo fundisho la kanuni. Kama hatuwezi kukifanya katika miaka saba, kipito chetu kinakuwa miaka 21. Miaka 21 hiyo iligawanywa katika madaraja tisa. Kwa sababu gani hivyo? Kama tungekikaribia chote kwa mara moja na tungeshindwa, hapo tungepoteza kila kitu. Lakini, kama tutaenda hatua kwa hatua, toka daraja moja kidogo kidogo hadi lingine, hapo hatuwezi kupoteza kila kitu kwa mara moja. Tunaweza kuviunganisha na kama tutapata ushindi katika kila daraja, tunaweza kupanda kwenye kiwango kifwatacho. Tulikuwa tunafuata maarifa ya vita hiyo kwa hiyo ingawa mafwatano ya mambo yanaweza kuonekana yakichanganyika, maongozi ya Mungu yakisogea mbele kwa kutulia kuelekea kwa utimizo wake. Shetani ni mwenye busara sana pia njia yake ni ya kutia mashaka. Kwa kuwa yeye ni mnadhifu, yeye anaweza kuvuta kwa hila shauri la Mungu kwa kujiweka mwenyewe katikati. Kuna watu wengi ambao wanavutwa kwa hila hadi mbali kwa kuongozwa na tamaa yao binafsi. Mtu wa aina hiyo anafanya madhara mabaya kuliko yote ndani ya dini. Mahali pa kuanzia kwa shuguli zote za Kanisa ni Mungu, na mtu kama huyu ataongea kuhusu dhumuni la taifa au Mungu, lakini atalidharau na kufanya vitu kwa faida yake binafsi. Yeyote atakae kusanya fesa/fedha za mtu mwingine kwa kusudi la uma na kutumia fedha hizo kwa kinyofu kwa ajili yake mwenyewe ni mwizi. Kanuni hii inatumika kwa yeyote anaedai vitu vya uma kama mali yake binafsi bila kupata ruhusa. Mtu kama huyu atateketezwa toka ndani.

Tafadhali muelewe wazi kwamba ukombozi unakamilika kwa njia ya malipizi na hii ndiyo njia ya kufikia ukamilifu. Na nyie, Washirika wa Kanisa la Umoja je? Ninaongea siku zote kwa njia ya waziwazi na ninaweza kuadhibu kiongozi moja wa Kanisa wakati wa hotuba. Ile mfano wa ukombozi kwa njia ya malipizi. Ninapo muadhibu mtu huyo hadharani ya watu, yeye anawakilisha dunia, na kama atanisikiliza na kukubali kile ninachosema, yeye ana uwezo wa kushinda tatizo. Ninapofanya kitu kama hicho, kwa uhakika tatizo linakuwa dhahiri. Aina hiyo ya rada hadharani ya watu ni mfano mzuri zaidi wa ukombozi kwa njia ya malipizi. Nini dhumuni la malipizi? Ni kwa ajili ya ukamilifu-ukamilifu wa mtu, ukamilifu wa familia, ukoo, taifa, dunia na ulimwengu. Na nini tukio la ukamilfu wa ulimwengu? Tukio la mwisho ni kumfanya Mungu huru.

DESTURI KWA WALE WANAOFUATA NIA YA MUNGU

Kwa sababu nilielewa jambo hili, nilikazania kabisa uvumbuzi wa njia ya ukombozi kwa malipizi. Njia yangu ya maisha ilikuwa ya kutojali theluji, upepo au mabadiliko ya msimu; maisha yangu yanaweza kujumlishwa kwa neno moja-(unyonge) shida. Ninatembea njia ambayo hakuna mtu yeyote ila Mungu anaweza kuelewa. Mnapoomba kwa moyo juu yangu na nia ya Mungu, sharti mlie zaidi na zaidi. Mkiuliza Mbingu mie ni nani, mtalia na dhoruba ya machozi itabubujika (itatiririka) juu ya uso wenu. Mtasikia kichomi kama hicho moyoni mwenu-kichomi kinachosababisha maji kama hayo kutiririka. Lakini kwa nini iwe hivi? Kwa asili, mlidhaniwa kusimama katika nafasi ya aina tofauti. Ikiwa ulimwengu wa utamaduni wa Ukristo ulinipokea, katika miaka saba wakati wa umri wangu wa miaka 30 na kadha-ningeweza kurudisha dunia katika milki ya Mungu. Mambo ninayoyafundisha sasa hivi hayakuanza juzijuzi; nilianza katika njia hii kwa kufichua asili kabisa ya ukweli huu. Hapo ndiyo niliweka msingi, na nilikuwa naleta mafanikio katika maisha yangu hadi nafasi hii sasa ninapowafundisha nyie mambo haya. Hili sio wazo la kuwazika tu. Kwa kweli nilifanya kile ninachowafundisha sasa. Nisingeweza kuongea na nyie kabla ya kuyafanya haya, kama sivyo mnaongozwa katika dunia ya Shetani.

Nyie washirika wa Kijapani lazima sasa mfikie juu ya maisha yenu. Mlikuwa mnafanya kazi ngumu hadi muda huu, kwa kunifuata, na miezi, miaka-katika hali nyingine miaka 10 au 20 imeshapita. Mnapogeuka na kuchungulia juu ya maisha yenu ya imani, mnapata nini? Nilikuwa na panda kwa shida kilele cha malipizi, refu kuzidi Himalayas, mpando mgumu kuliko wa mtu mwingine yeyote katika historia. Sasa ninawaangushia kamba toka Japan kwa wengine wote duniani. Sisi sote tunafanya kazi ngumu ya kufanya kutisha. Iwezekanavyo, nyie ambao mko katika nafasi ya kufanya hivyo, mngevuta kamba pamoja nami na kunisaidia ili muweze kulegeza kutanuka kwa kamba ile. Lakini je mlikaza kamba hiyo wakati wo wote badala yake? Je hamkulalamika kwa kujifikiria, na kulaumu, kwa kusema vitu kama, "Baba wa Korea tu"? Ningewazia Korea tu, nini kingetokea? Ningesha kamatwa katika dunia kiroho zamani sana. Mtu kama huyu hahitajiki kwa dunia hii. Baada tu ya ukombozi kwa njia ya malipizi wa dunia yote, baada ya nyie kusafisha kila ktu, ndio mnaweza kurudi kwenye asili yenu na kufikiri kuhusu watoto wenu, familia yenu au taifa lenyewe. Hii ni njia peke yake kwa mtu alieamua kwenda njia ya Mungu. Hii ni kwa mtazamo wa maongozi. Mkifikiri mambo tu kwa kuzingatia nyie wenyewe, familia yenu au taifa lenu, hamtaweza kusaidia dunia.

Je mnaweza kweli kujionea fahari mbele za Mungu? Nilikuwa naongoza njia hii kama mvumbuzi kidunia wa ukombozi. Upeo gani mlikuwa nao katika uhusiano wenu na mimi? Msipojiona wazi nyie wenyewe na kuweza kubadilika leo, hamwezi kuwa wamahali bendera la ushindi wa kesho. Na kiwango cha taifa, Japan inasimama katika nafasi ya taifa Eva katika uhusiano na taifa Adam. Kwa hali hiyo, msingekuwa na hata chembe moja ya shaka/tuhuma au kero, au kunipa ugumu wowote. Tukikumbuka kwamba utamaduni wa kihistoria wa kweli ulivunjwa na Eva alieanguka, hakuna budi nyie kumpa hata taabu ndogo roho ya Baba wa kweli. Nyie mnawakilisha dunia na walimwengu wote kwa ujumla; ile ndio nafasi ya Japan kama taifa Eva. Je mnaelewa? Ujumbe wangu kwenu, msilalamike lakini mshuhudie pia msimame katika mstari wa mbele wa nia ya Mungu. Hata tusipoweza kutimiza upeo wa ukamilifu kwa wakati huu, tunaweza kuhakikisha kwamba baadaye(wakati ujao) tutaweza kuutimiza, kwa sababu tuna kanuni hii. Na nyie je? Je mnataka kulikamilisha siku moja baadaye sana, au mngependa kutimiza ukamilifu wakati wa muda niishipo? Kwa kufanya hivyo lazima kufanya kazi kwa kunusuru maisha yenu(kwa kuweka maisha yenu mashakani). Wale ambao walizalia siku za nyuma(zamani) na walikuwa na imani ya kidini hawawezi kuzaliwa tena katika zamani zetu, ingawa wanapenda kuwa. Kwa hivyo, wanasubiri kwa kutazamia sana na kuchungulia toka dunia ya kiroho, kwa kujua kwamba huu ni muda tunu zaidi katika historia, ambao hauwezi kubadilishwa na wakati mwingine wo wote. Mnaelewa nafasi hii, mnalazimika kuwa na shukrani sana kwa tendo la kwamba mnapokea maneno moja kwa moja toka kwangu duniani. Mnapokea elimu moja kwxa moja toka kwangu na mnakamilisha kusudi la Mungu.

KILELE CHA UDHALIMU.

Kilele cha mwisho na juu cha udhalimu na kiwango cha dunia ilikuwa mwaka 1976. Tulifika kileleni wakati wa muda wa mkusanyiko wa Washington Monument(Mnara wa Washington). Kwa kuwa nilielewa jambo hili, nilituma ma missionari/watume duniani kote mwaka 1975. Kama watume wote walikuwa wajapani, wangekuwa makundi ya watu wa mashariki tu kwa kweli. Kama walikuwa watu wa Amerika tu, wangukuwa na kundi la watu wa magharibi tu kwa kweli. Kwa hivyo, niliwaamuru ili waweze kuwakilisha dunia nzima. Kwa kila nchi ya utume, nilituma mtume wa Kijapani ambaye aliwakilisha mashariki, mjerumani ambaye aliwakilisha America ya kaskazini na ya kusini. Hapa walikuwa wa wakilishi wa dunia, pamoja na wale wa Revereland Moon wa Korea. Wajapani, Wamarekani na Wajerumani wote walishiriki mazingira sawa na wote watatu waliitwa wa Mooni. Wasingekuwa na mwongozo kutoka kwangu, bila shaka wangeomba na kuachana. Mtume wa Kijapani angeweza kusema,"Japan ilitangulia kupokea baraka, kwa hiyo mimi niko katika nafasi ya Abeli." Mmerikani angeweza kusema,"Amerika ni taifa inayoongoza dunia ya Kidemokrasia, kwa hivyo kwa mtazamo wa kiutamaduni, mimi ndiye bora." Halafu mjerumani angeweza kusema,"Upuzi! Wajerumani ni nadhifu zaidi. Sisi ni watungaji bora zaidi, sisi ni wachanganuo na wa akili." Kila mmoja wao angedai kwamba yeye ni bora na kwa hiyo yeye ndiye mtenda. Kwa sababu hiyo, busara ilibidi iwe ya kwamba hakuwepo mtenda yeyote. Kama hakuna mmoja wao wa kudai uongozi wake, hapo Mungu angeweza kuwasaidia kwa uhakika. Kwa hivyo nilisema wazi,"Kama wote watatu mtaungana kabisa, Mungu atawasaidia kwa uhakika na mtaendelea. Kama mtagombana, kamwe hamtakuwa na upole. "Na hali ilionyesha sawia kile nilichokisema. Hakuna kosa ndani ya kanuni. Watume walienda duniani kote na ulimwengu wa kanuni ulipanuka kwa mataifa 130. Kwa hivyo, udhalimu ulisambaa duniani kote kama mwavuli; wamerikani wengi walikuwa wanaomba ufukuzob wa Reverend Moon kabla ya mkusanyiko wa Mnara wa Washington, lakini haukutokea. Nilipigana na kupata ushindi. Mwaka 1976, muda kilele wa udhalimu dhidi yangu, dunia ilipokea wakati mpya. Halafu, tarehe 23 Februari 1977, na msingi wa azimio la kuzaliwa kwa Wazazi wa Kweli nilitangaza wakati mpya.

Ninawezaje kusema hivi? Ni kwa sababu kileleni kwa udhalimu (wa) kidunia, nilikubali taabu na nilitembea mbele kwa ajili ya Mbingu na kwa ajili ya dunia. Halafu dunia ya Kicommunisti iligawanyika. Miaka mitano toka hapo Japan ilisogea mbele hadi kiwango cha dunia. Eva anapoinuliwa(juu), Adam pia anaokoka kwa njia ile ile. Mungu alifanya busara kutangulia kuinua Japan.

KAZI YA JAPAN KAMA TAIFA EVA

Mungu anapoangalia kando kando ya Japan akitafuta baadhi ya watu ambao anaweza kuwakabidhi (ma) jukumu, yeye anaona wale ambao wanaonekana wanyenyekevu, wale ambao wanaonekana kama wasiofaa kwa wajapan wengine. Wale ndio wa Mooni. Tunapo kuja kuwafahamu, tunaona kwamba wao ni waadilifu sana pia ni washarifu sana kwa ndani(kiroho). Wanatoa kila kitu na wanafanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya taifa na dunia, walakini hawaombi kamwe malipo. Basi, watu wameanza kuona kwamba wao kweli ni wa thamani. Mama mzazi sharti achukue jukumu lake la kihistoria/kimajaliwa. Japan ni Eva, na Eva anatakiwa lazima alishe watoto wake. Ni kwa nani Eva alianguka alimpa maziwa yake kwanza? Kwanza kwa Kaini na baadaye kwa Abeli. Mabinti wake hawakutajwa bado. Ingawa wanawake walikuwa wanaishi, walitendewa vile kama hawakuwako na hadi sasa hawakuweza kulalamika. Wale watoto waliolelewa kwa maziwa ya Eva walipigana/waligombana wao kwa wao kwa sababu walikuwa na tabia yenye kupigana. Katika ukombozi kwa njia ya malipizi, Yakobo na Esau waligombana wao kwa wao wakiwa tumboni kwa mama yao. Uhusiano wa Kaini na Abeli sharti kurudi ndani ya tumbo la uzazi la mama na kukombolewa tena kuanzia na nafasi hiyo. Kwa sababu hiyo katika kipito cha ukombozi, wakati maongozi alikuwa na mimba ya mapacha, hawa hawakutakiwa kupambana ndani ya tumbo la uzazi, lakini afadhali kukumbatiana. Baada ya wao kuzaliwa, moja asingejaribu kutangulia kunyonya maziwa. Kila mmoja wangesema,"eti wewe tangulia." Wanapopishana kunyonya maziwa mara nyingi katika siku, wangependana wao kwa wao bila nung'uniko. Eva lazima azae watoto kama hawa.

Kwa kuweka/kutimiza sharti hili katika taifa la Eva, masharti ya ukombozi na kiwango cha dunia yanaweza kutimizwa. Wote wa aina ya Kaini na Abeli baina ya Wajapani msikilize maneno yangu vizuri sana. Wale wanaosikiliza kidogo kulikoni Wajerumani. Zamani, Ujerumani ulikuwa unatawala/ na nafasi ya mtenda juu ya Japan. Endapo kaka mkubwa anasukumwa na nafasi ya mtendwa/ya kutawaliwa, yeye hapendi jambo hili. Wale ambao wanasikiliza zaidi kuwa na nafasi ya kutawaliwa/mtendwa ni Wajerumani. Juu ya hayo, kati ya Kambi la Abeli, yule ambaye anashida zaidi, yule ambaye anadai uhuru wake wakati anamwita Mungu, na ana mapinduzi ya kiroho zaidi, ni Wamarekani. Nani anawakilisha dunia? Wajerumani na Wamarekani ambao wanasimama na nafasi ya mapacha sio kwa kweli marafiki sana/wapole sana. Kweli, ni maadui kwa mazoea pia historia ya kila mmoja wao ilikuwa historia ya mapigano. Kwa maana hiyo Amerika na Ujerumani wanafaa katika mtazamo wa kanuni wa kuwa maadui. Taifa la Adam, Taifa la Eva na taifa la malaika mkuu nazo pia ni maadui. Zote ziligawanywa mahali ambamo walitakiwa kupata kuwa mmoja kwa kuwapangilia mara nyingine tena, yatupasa kuanza toka hali inayofanana (iliyosawa). Korea, taifa Adam, ilikuwa adui wa Japani, taifa Eva. Japani na amerika walikuwa maadui; Amerika na Ujerumani walikuwa maadui-wao wote walikuwa maadui. Nilikusanya maadui wa kihistoria hawa na kuwaambia waungane kuwa mmoja kwa kupokea maziwa ya mama, kwa kuongozwa na nguvu za upendo! Nyie wamarekani, wajerumani na wajapani hamuwezi kurudi kwa nafasi ya Adamu msipopata kuwa mmoja wote watatu. Huu ndio mtazamo wa kanuni kwa kadiri ya ukombozi kwa njia ya malipizi. Kwa njia ya anguko, Mungu, Adamu na Eva wakawa maadui. Adamu na baba, mama, na watoto, wote wakawa maadui. Ulimwengu wa kila mmoja wa maadui hawa ulipopanuka, wakafanyiza tunda moja. Kile kilichotokea(mwishoni) hatimaye ni kwamba taifa adam ilijitokeza katika dunia ya kishetani, vile kama taifa Eva, na taifa malaika mkuu. Knyume nazo kulikuwa na taifa Adam upande wa Mungu, vile kama taifa eva, na taifa malaika. Kambi hizo mbili zilipigana wao kwa wao katika vita ya kiwango cha dunia wakati wa vita kuu ya pili ya dunia wakiwa kama mataifa mhimili na matifa marafiki.

Mataifa mhimili wakiwa upande wa Shetani walianzisha vita ile. Japani, ambayo ilikuwa taifa Eva ya kishetani, ilishika mashariki, sana sana Korea. Wazo la ulimwengu ustawi kwa pamoja wa Asia ya mashariki kuu lilijitokeza, kwa kutangulia mbele ya nia ya Mungu, kuwa kama ubisho kwa nia asili ya Mungu, na upande wa kishetani Dini la Japani la Shinto inatambua"Miungu milioni nane", lakini Mungu mwasisi wa taifa Eva, ni amaterasu-Ominokami, Mungu wa aina ya kike. Kwa upande wa Mungu, Uingereza ilikuwa taifa Eva. Amerika ilizaliwa toka kwa Waingereza, kwa hivyo amerika ni mtoto wa Eva, na siku zote anamfuata. Lakini kama Amerika ataendelea kufuata Uingereza wakati wote, sio vizuri. Mfano mmoja ulikuwa vita ya visiwa vya Falklands. Amerika angetakiwa kwenda njia yake kwa ushupavu bila Uingereza. Siku zijazo, lazima asimame kama taifa Adamu chini ya upeo wa Mbinguni. Katika vita kuu ya pili ya dunia, taifa Eva lililokombolewa ilikuwa Uingereza na taifa la kimalaika mkuu lililokombolewa ni Ufaransa. Kushindana na haya, kulikuwa na taifa Adamu la kishetani ambalo ni Ujerumani, taifa Eva ni Japan, na taifa la kimalaika mkuu ilikuwa Italia. Wote watatu kwa pamoja walitunga msingi wa nafasi nne chini ya kusudi la Shetani katika nafasi ya juu, wakati Mataifa marafiki walitunga msingi wa nafasi nne chini ya Mungu Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita ya kushinda na kiwango cha dunia. Baada ya upande wa Mbinguni kutwaa ushindi, dunia ya kishetani iliweza kurudihswa upande wa Mbinguni. Katika hatua ya mwisho ya upande wa Shetani na kiwango cha dunia, communism ikaja kuwako.

Communism ni nini? Communism ni jaribio la Shetani la kuiga kipeo cha Bwana wa Ujio wa pili, kabla Mungu hajaweka bado dunia yake. Tukiangalia kile Stalin alichokifanya, tunaweza kuelewa wazi sehemu hii. Yeye alijaribu kuunganisha dunia nzima. Lakini Communism sasa imeshakua kwa kupîtia vizazi nane, toka Marx, hadi Lenini, Stalin, Malenkov, Bulganin, Khrushchv, Brezhnev na Andropov, ambaye ni kizazi cha nane. Wamesha fika mwisho; kuanzia sehemu ya nane, chochote wanaweza kufanya ni kushuka. Bwana wa Ujio wa pili analeta dhumuni la kiroho umoja wa dunia nzima, wakati communism, na msingi wa materialism, inatoa lengo la kuungamanisha dunia na kiwango cha mwili kwa kulingana na kanuni, kama Ukristo unapata kuwa mmoja kimwili wameungana, msingi wa shetani kuwepo utatoweka. Mungu ataongoza ulimwengu wa mtenda na wa mtendewa, basi hakutakuwepo ulimwengu wa kubadilishana kwa shetani kuuongoza. Mwisho communism itarushwa mbali kabisa. Kama dunia ya kidemokrasia ilimfuata Bwana wa Ujio wa Pili baada ya mwaka 1945, dunia ingeungamanishwa katika kipindi cha miaka saba. Lakini hawakuungana na Masihi, badala nayo walimpinga. Kwa sababu hiyo, walisimama mbeleni mwa mapambano ya upinzani na kususdi la Mungu. Kwa sababu hii dunia nzima, pamoja na communism, demokrasia, Ukristo, Uyuda, Buddhism na kadhalika, walimpinga Masihi na kiwango cha mtu mmoja, na kiwango cha familia, na kiwango cha ukoo, jadi, taifa na dunia. Wao wote walimpinga. Kwa sasa hivi, tuna pambano mahakamani kati ya serikali na Revereland Moon, mwenye kudai ni amerika, ambayo inawakilisha dunia huru nzima, wakati Reverend Moon ni mtu mmoja. Ni nani atashinnda? Sasa ni muda muafaka wa vita ya kushinda, wakati wa ushindi au ushinde. Tumefikia kilele kwa hatua ya mwisho ya Vita.

MATAIFA MAKUU MANNE KATIKA MAONGOZI

Leo ni tarehe 3 April, siku ya tatu katika mwezi wa nne. Kwa mtazamo wa kanuni, namba 4 inawakilisha dunia na namba 3 inawakilisha hatua tatu ya mwanzo, kukua na ukamilisho. April 3 ni siku ya kustaajabisha. Na 1983 inajumlisha namba 21, yaani 1+9+8+3=21. Kwa hivyo, kati ya siku hii siwezi kujizuia kuongea juu ya somo la malipizi timilifu, ukamilifu timilifu. Kwa kuwa nimeisha wafundisha mambo haya, ni jukumu lenu kutembea njia hii, kama hampendi kwenda, basi msiende. Kiini cha shughuli yangu ni nini? Je ni Ukristo wa Korea? Hapana, ni amerika, ambae kwa msingi ni taifa ya Kiprotestanti. Kati ya Ukristo duniani, Waprotestanti ni ma-Abel. Wakati wa matengenezo ya Kanisa la Kiingereza, Kanisa Katoliki liliwadhulumu Waprotestanti. Baadaye, Waprotestanti walitoweshwa nje ya ulaya. Mwisho wake, nchi ya wa roho ya kiprotestanti ilitungwa Mmerikani. Kwa kuhesabu toka 1976, 1985 ni mwaka wa 210 . Vita ya kushinda lazima kuishinda, chini ya uongozi wa Rais wa 40, ambaye ni Rais Regan. Kwa wakati wa kihistoria huu, nilishatoa mari ya uhamasishaji. Shirika letu sio la kuharibu ni la kuunganisha na kuvuta pamoja dunia nzima. Kwa hivyo, na nafasi hii yatupasa kutimiza sio muunganisho wa jadi peke yao, lakini pia ni muunganisho wa dini mbalimbali za Mashariki na Magharibi. Historia zote za mataifa yote zimekazana upande wa pointi moja. Huu ni mwaka 4318 katika historia ya Korea. Namba 18 ni 6 mara 3 na 6 ni namba ya Shetani. Mungu ni mwenye maarifa ya Sayansi, na tena, mwenye kuwepo kwa mahesabu. Kwa hivyo, ukombozi kwa njia ya malipizi iliendelezwa kwa kutumia masharti mengine ya mahesabu. Malipizi yana amrisha kipindi fulani cha muda, kiongozi, na sadaka kuu tatu. Kwa kuptia Baba wa Kweli, masharti lazima yatolewe kwa kupitia taifa Adam, taifa eva, na taifa malaika mkuu. Na nafasi hii yatubidi kutoa sadaka wake na kiwango cha dunia kwa Mungu. Lazima tukomboe dunia nzima kwa kupata sahihi ya ushindi. Nani anaetakiwa kutoa sahihi hii ya ushindi? Mungu hafanye mambo haya, na hata Masihi hafanyi hivyo. Ni shetani ndiye anefanya mambo haya.

Mataifa makubwa manne yalichaguliwa na Mungu kwa kuwakilisha mataifa yote ya dunia. Korea ni taifa Adam na Japan ni taifa Eva. Isingekuwa kwa kushindwa kwa Ukristo kunifuata, Uingereza ungekuwa taifa Eva. Kwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya dunia, taifa Adam upande wa Mungu ilikuwa America, taifa Eva ilikuwa Uingereza; na taifa malaika mkuu ilikuwa Ufaransa, lakini Shetani alishambulia ulimwengu wa uamaduni/uungwana wa kikristo. Upande wa Shetani, Ujerumani ilikuwa Adam na Japan ilikuwa Eva wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Huko Korea, kwa sababu ya uasi wa Ukristo dhidi ya Mungu, Korea Kaskazini, kule ambamo kijiji changu kilipo, ilishambuliwa na Shetani. Basi, kichwa kilishambuliwa na Shetani, lakini mkia-Korea Kusini, iliokoka. Sasa Shetani anashika kichwa cha Adam na mkia wa malaika mkuu. Hawa ndiye Korea Kaskazini na Kusini, au kwa latitudo, na Ujerumani katika Mashariki na Magharibi, au longitudo. Shetani anashika Korea Kaskazini chini ya Pyong Yang na Ujerumani Mashariki chini ya Berlin. Kama tatizo la Communism litatatuliwa huko Korea, basi moja kwa moja litadhoofisha mbali huko Ujerumani. Kwa njia hii, communism kwa ujumla itaanza kufa. Huko korea Kaskazini, Kim II Sung anaitwa "Baba", lakini kati ya Kanisa la Umoja huko Korea Kusini, Mzazi wa Kweli ndiye Baba halisi, basi, kwa wakati huu kuna ma-baba wawili na kuna watenda wawili. Upotovu huu utarekebishwa kama malipizi yamelipiwa kwa ajili ya dunia nzima; hapo dunia itapita moja kwa moja. Kama walimwengu wote wameungana na Mungu na wanataka kwa hamu kujitoa mhanga, na kuwatamkia wengine, hapo tatizo la mapigano duniani litaisha. Kwa njia ile, dunia jinsi ilivyo sasa hivi itaisha. Kwa haya, America pia inakaribia mwisho, vile kama Uingereza, Ujerumani, na mataifa mengine.

Buddhism, Islam, Ukristo, na dini zote zinakaribia mwisho, nazo pia. Madaraka yote, yakiwa ya kiuchumi au kisiasa, hata familia, zote zimekuwa zimechafuka. Utaratibu batili wa upendo, ambamo watu wanajipenda wenyewe kuliko hata Mungu na wengine, wamekuwa wa kijiharibu; basi maovu ya dunia yamekuwa yakivunjwa. Kwa hivyo, kwa wakati huu lazima tutunge utaratibu mpya wa upendo. Masharti ya malipizi pamoja na uaminifu lazima yalete umoja, kokote Mbinguni na nchini. Baada ya kiini cha upendo kuwekwa, utaratibu wa upendo unaongozwa na Mungu unapanuka mpaka kufikia kiwango cha dunia. Kwa njia hii Ufalme wa Mbinguni mpya unaenda kukamilishwa duniani. Shirika la Umoja limesha fahamu mataifa makuu ambao Shetani anatamani na anataka kwa nguvu zaidi kuongoza. Kwa mtazamo wa mambo ya dunia leo, Korea ni taifa la muhimu zaidi huko asia. Japani ni taifa kisiwa la bahari la muhumu zaidi. Zile nchi ambazo zinakutwa kandokando na Bahari Pacific na zinatamani kuwa taifa kubwa baharini zinahitaji Japan. Utamaduni wa Magharibi lazima uende barani Asia kwa kipitia Bahari Pacific, na kwa sababu hiyo unahitaji uhusiano na Japan, ambae ni njia ya kwenda barani Asia. Kwa hivyo, Japan anatakiwa kuheshimika. Tena, Japan kama taifa Eva, sharti aelimishe watu toka sehemu zingine zote za dunia. Hii ndio sababu ya Japan kubarikiwa sana sana katika miaka30 au 40 iliyopita, kwa mali, kwa kwenda barani Asia, mtu anaweza pia kipitia mkono wa nchi ya Korea, lakini sio rahisi kufikia mkono wa nchi nzima kwa meli. Kwa sababu hiyo mradi wa kufanya shimo refu la kupenya ndani/kupitia chini na njia kuu kote kote Asia. Humo Korea, kwa hivyo, Shirika la Umoja limepata kuhitajika zaidi na zaidi kwa tatizo lo lote la kidunia hata la nyumbani.

Muda wa kupendeza umekuja. Ukamilifu hauwezi kutimizwa bila ukobmozi timilifu kwa njia ya malipizi, na ile inakamilika kwa njia ya umoja. Ukamilifu wa wote unakuja kutokana na malipizi yaliyolipiwa na wote. Kwa hivyo, yatupasa kumaliza na kwamba malipizi yamelipiwa kwa kutimiza umoja baina yetu/miongoni mwetu.

MWISHO WA DINI.

Kama maadui wanaungana, na kama wanatoa mhanga umoja wao kwa Mungu na Mungu anaukubali, hapo kusudi la dini itakamilika. Mpaka hapo, ni wale tu ambao walikuwa upande wa Mungu walikuwa wanatolewa sadaka madhabahuni. Lakini leo, kwa njia ya Umoja wa maadui, wale ambao wako upande wa Shetani na wao pia wanatolewa sadaka madhabahuni. Mara tu watakubalika na Mungu, kusudi la dini itakamilika. Dini yenyewe haitahitajika tena. Dini linakuwako kwa kumaliza kutenganishwa kwa mtu na Shetani, lakini kwa umoja kamili na upendo miongoni mwa maadui haja hiyo haitakuwa inatolewa kwa Mungu, yeye atazikubali. Lazima tufanye hivyo na kiwango cha dunia. Ile ndio sababu sharti nianze na nafasi ya kuwapenda maadui wangu. Ile ni kanuni. Msingi wa Ufalme wa Mbinguni unahitaji kuchipuka toka makao kabisa ya Shetani. Kwa kufanya hivyo, lazima mteswa na wale ambao wako upande wa Shetani, na lazima mwapende kwa kulipa ili wajisalimishe kwenu bila tatizo. Kama watawapiga nyie ambaye ni waadilifu, basi lazima walipe kwa hiyo. Ile ni kanuni ya ulimwengu. Kwa njia ya malipo kama hayo, mnaweza baadaye kukomboa mahusiano. Lakini kama mtarudihsa kipigo kama Shetani, hapo mahusiano hayawezi kukombolewa. Mnapopigwa vile lazima mkubali dhoruba kabisa. Kwa kukomboa njia hiyo kimwili, mnaweza kukomboa viasili vya muhimu zaidi ndani ya Shetani. Hivyo, kile ambacho mnapanda kwa uhakika kitavunwa. Ni kazi ya Bwana mkubwa kutenganisha waovu na wema, na kuweka kile ambacho ni kibaya ndani ya ghala la waovu na kile ambacho ni chema ndani ya ghala la wema. Kati ya dunia hii, mbegu mbili zilipandwa, moja ni mbaya na ingine ni bora. Mbegu nzuri itaenda kwenye ghala ya Kimbingu, lakini mbegu mbaya itachomwa na moto. Sasa ni majira ya kuvuna, na dunia katili/ya kishetani iko katika machafuko. Kwa sababu hiyo, yatupasa kutoa umoja toka ndani ya machafuko na kuunganisha watu wa mbegu/jadi zote. Dunia ya anguko ni dunia ya ubinafsi. Hakuna umoja kati ya wazazi, watoto, jamii za watu, au mataifa. Lakini Shirika la Umoja inaunganisha watu na viwango vyote. Shirika letu linaenda njia ambayo ni kinyume na njia ya kawaida kati ya taifa moja au jadi moja, lakini ndani ya Kanisa la Umoja, ni kinyume chake ndio kinajitokeza mara nyingi. Mjapani asingeweza kufikiria kamwe kuozwa na Mkorea au mweusi, lakini sisi tunafanya hayo bila wasiwasi. Tunafanya hayo kwa ajili ya nini? Kuunganisha dunia, na kumrudishia Mungu dunia katili ya ufarakano, ambaye kama sivyo ingeteketezwa. Katika utaratibu huo, nani atalipa malipizi? Ni Shirika la Umoja na wale watu ambao wamo katika mkondo mkuu wake. Mimi ndiye kichwa cha mkuki(kiongozi, mapenzi) cha hcma kile, na ninatembea njia ya malipizi kwa niaba ya dunia. Ninapolipa malipizi na kiwango cha mtu mmoja, nafanya hivyo kwa niaba ya walimwengu wote. Nilianzisha Shirika la roho ambamo watu wanajisikia hata kama kumpokea mwanamke mwenye uso mbaya zaidi duniani kuwa kama mke wao. Ile mnalipa malipizi kwa kuanzia toka na roho adilifu/nyenyekevu kama hiyo, hamwezi kamwe kukamilisha dhumuni la ukamilifu kama mume mmoja. Ila wanawake wote, wakiwemo mabibi, na mabinti, na wanawake katika dunia ya kiroho, wanawapenda hasa, basi hamwezi kamwe kukamilisha dhumuni la ukamilifu wa mume mmoja. Mnaweza kusikia kitu kama hicho kwa mara ya kwanza.

Nyie wanawake Wajapani mlinipenda kama baba au kaka au hata kama mume wa Kimbingu kabla ya kuozwa, au sio? Ile ni tukio la kiroho. Kwa njia ya dunia kiroho, mliweza kupata uzoefu wa kutembea(mkono kwa mkono) na mimi. Hii ni kwa sababu mume mmoja anahitaji kukomboa pamoja na kuunganisha aina tatu za upendo; yaani, upendo wa mama, upendo wa mke, na upendo wa dada. Haya yote yalipotezwa kwa kuanguka kwa Adam; kwa hivyo, lazima yote yatakaswe. Kwa njia ya Adam mmoja alietakaswa, masharti ya malipizi kihistoria kwa ukombozi wa ukamilifu wa mtu mmoja yanapaswa kutimizwa na kiwango cha dunia nzima. Kwa sababu hiyo, wanawake wote wa aina mbalimbali sharti waje wote kumpenda kitakatifu ili Shetani atawaliwe. Adam mtakatifu lazima awaongoze wanawake wote vizuri lazima yeye hata adaishe wanawake wamalaya kwa kuwafundisha njia ya kweli. Lazima wampokee kama mtu wa kweli. Ingawa anaweza kujaribiwa, sharti asishindwe; badala yake lazima ashinde juu ya majaribio. Haidhuru mrembo gani mwanamke anaweza kuwa au jinisi yeye anaweza kujaribu kumtongoza, sharti yeye asianguke. Yampasa kuimarisha desturi ya aina ile. Kama sivyo, yeye hawezi kamwe kutimiwa kusudi la ukamilifu la mtu mmoja.

KUBUNI UKAMILFU WA MTU MMOJA.

Baada ya kukamilika kwa mtu mmoja Adam kutimizwa, Eva anatakiwa kuumbwa tena, kwa sababu kwa asili Eva aliumbwa kufuatana na kifani cha Adam. Kwa kuwa Adam hakuweza kutimiza wajibu wake wakati Eva alikuwa anaanguka, Shetani aliweza kufaulu katika kumpevusha. Adam aliekombolewa lazima sasa amnyan'ganye Eva kwa Shetani. Mungu aliandaa msingi kidunia kwa sababu hiyo. Eva mpya lazima awe chini ya umri wa miaka 20, vile kama alikuwa Eva asilia. Kwa sababu hiyo, Mama wa Kweli alikuwa msichana safi wa miaka 17 tulipobarikiwa.

Miaka saba ya kwanza ya ndoa yetu ilikuwa kipindi cha utii yakinifu kwa Mama. Katika kila njia, yalimpasa kunitii. Kwa utaratibu huo, siku ya wazazi, siku ya watoto, siku ya Vita vyote, na siku ya Mungu iliweza kuimarishwa. Hadi siku ya Mungu ilipoimarishwa, wazazi wa kweli walilazimika kuhuzunishwa na aina zote za matatizo ya kiroho na kulipia malipizi kwa ajili ya kushinda masuto ya Shetani. Siku ya Mungu ilimaanisha kuanza kwa Adam na Eva wakamlifu. Mwaka 1968, kuanzia na msingi wa siku ya Mungu, Kanisa la Umoja lilituma familia zote hadi wa 124 katika kila ncha ya Korea Kusini kwa miaka mitatu, na walidhulumiwa sana. Niliwaamuru wanafamilia wote kwenda kwenye mstari wa mbele kuongea kwa miaka mitatu. Hii ilikuwa malipizi ya kifamilia na kiwango cha taifa. Watoto wengine walilazimika kupelekwa kwenye nyumba ya watoto yatima, na wengine walitumwa kwenye majumba ya wazazi wa umimi . Chini ya malipizi haya ya miaka mitatu na juu ya ukamilisho wa msingi wa familia na kiwango cha taifa huko Korea, niliweza kuja Merikani kipindi hiki kilianzishwa ili kulipia malipizi matatizo yote ya zamani ya familia. Kwa sababu ya hiyo, nilidhulumiwa, hata na mafamilia ndani ya Kanisa ya Umoja. Walisema, "Hivi sasa tu ndio tumeanza maisha ya ndoa. Tumefanikiwa kupata ka-nyumba kadogo na kukusanya masufuria na matawa kidogo, vijiko na vijiti na vyombo na mapambo ya nyumba, ingawa havipo vizuri sana; lakini unaenda kuvunja kila kitu. Kwa nini unatufukuza nje hivi?" Malalamiko kama hayo yalitolewa, lakini nilijibu, "Nendeni nje." Kwa sababu gani nilikuwa mkali kiasi hicho? Kwa sababu ya kanuni. Ila unalipa malipizi na kiwango cha jamii, huwezi kamwe kuimarisha msingi kwa familia. Na ili kuweka msingi kwa familia huwezi kamwe kuweka msingi kwa ukamilfu wa mtu. Ila unalipa malipizi na kiwango cha juu zaidi, huwezi kamwe kuishi kwa raha kama mtu binafsi. Ile ni amri kali.

Baada ya kipindi cha miaka mitatu kumalizika, nilibariki familia 777 ili kuunganisha msingi uliojengwa na wanafamilia na dunia nzima. Shetani alijua vizuri misingi hiyo ilishawekwa. Baada ya kuondoka Korea kwa ndege, nilisimama katika mataifa matatu-Japani, Canada na America-ambayo, pamoja na Korea, ilifanya msingi wa nafasi nne. Nilifika Merikani tarehe 18 December 1971. Kwa wakati ule, kundi letu la wa-"Malaika wadogo" (The Little Angles) ilikuwa inacheza kwenye Ukumbi wa Carnegie (Carnegie Hall). Hakuna mtu hata moja alienifahamu; na hakuna mtu mmoja ila Mungu na mimi mwenyewe alijua ningeenda Merikani. Hata Rais Kim (Young Whi Kim, ambaye alikuwa Rais wa Kanisa la Umoja Korea kwa wakati ule) hakujua. Walakini, kama mtasoma hotuba zangu nilitoa kwa wakati ule, mnaweza kuona madokezo ya kuondoka. Ilinibidi kukomboa njia ya mateso ya Yesu. Haipati miaka 31/2 Merikani, nilifanya safari ya kunena ya taifa zima kwa kusudi la kuhusisha Ukristo. Katika mwaka 1974, nilipokelewa kwa raha; nilipewa kama hati na tahadhari 1200, ikiwa pamoja na ufunguo wa miji mikubwa mingi. Ukristo huko Korea uliniasi, lakini Ukristo katika Umoja wa Mataifa ya America ulinipokea, vivi hivyo walilipia malipizi kwa ulegevu ule wa mwanzoni. Makanisa ya Kikristo ya America yalinipokea katika msafara wangu. Baada ya makaribisho kama haya, nilifanya nini? Tarehe 1 April 1975, nilituma IOWCs (kundi la kushududia la kimataifa) toka Magharibi kwenda Korea. Ma IOWCs haya walianza kazi zao kati ya Pusan. Tangu miaka elfu mbili, Urumi na viongozi wakuu wa Uyuda(Uyahudi)-judasim waliungana pamoja kwa kumuua Yesu. Lakini sasa kinyume chake kimetokea. America na Korea wamekuja pamoja kuungana na Kanisa la Umoja. Ukombozi kwa njia ya malipizi ulifanyika huko Korea. Katika mkusanyiko wa kisiwa cha Yoido, watu milioni 1.2 walikusanyika pamoja. Juu ya msingi huu tulifanya mikusanyiko ya Yankee Stadium na Washington Monument katika mwaka 1976.

AMERICA: KATIKA HAJA YA MSAADA.

Kwenye mikusanyiko hiyo miwili, nilisema kwamba America lazima inisikilize. Nilisema kwamba America ilikuwa ndani ya moto pia ilihitaji mzima moto; mtu mmoja toka nje ya taifa lazima aiokoe, na mtu huyo ni Reverend Moon. Ili kuponya ugonjwa wa America, utumishi wa Kanisa la Umoja na Reverend Moon sharti upokelewe. Kwa sababu nilisema hivi wazi/moja kwa moja wamerikani hawakujisikia kufariji; hata walikasirika. Toka hapa kaja wakati wa kumshambulia/kumshutumu Reverend Moon. Ndivyo, shughuli za kamati ya Fraser ilianza (kamati ndogo ya Halmashauri Kuu ya U.S. kuhusu mashirika ya kimataifa, chini ya uongozi wa mwakilishi Donald Fraser, Mdemocrat wa Minnesota, katika 1977 na 1978). Kuanzia 1977, na kuendelea, kipindi kimoja cha shughuli za bidii nyingi za chama cha wa-communist kilianza, vile vile na kamati ya fraser, ambaye walipigana na Bohi Pak. Yeye alikuwa ameshaoa kabla ya Baraka yake hivyo yeye likuwa na nafasi ya malaika mkuu. Na familia yake ilikuwa moja kati ya wanafamilia Adam, moja kati ya wanafamilia wabarikiwa wa kwanza. Mtu mmoja ambaye yuko katika nafasi yake sharti alete ushindi. Hukumu ilikuwa vita kweli. Yeye alikuwa anapigana moja kwa moja na Fraser pia utawala wa Rais Calter. Hakuna vita kama hiyo iliwahi kufanyika katika historia ya binadamu. Wakati wa miaka minne ya utawala wa Calter, hotuba yangu siku zote ilishambulia taratibu za Rais Calter, kwa kusema kwamba yeye alikuwa anauza dunia ya kidemokrasia yote na kuendeleza kusudi la communism. Kipindi cha Calter kilikuwa kigumu mno. Utawala huo ulinisuta kwamba sikuwa mtu mwingine isipokuwa ni mgaidi wa siasa wa kidunia na adui wa Amerika. Kama tukio lake, washirika wa Kanisa la Umoja duniani kote walikataliwa visa. Hiki kilitokea huko Japan na Ujerumani lakini haipiti miaka mitatu haya yote yatabadilika.

Shirika la Umoja linaleta ideologia ya nguvu sana. Walimu Vyuo Vikuu na wenye akili wakuu wengine sasa wanajikusanya kwa kunisaidia, wakati vyama vya communist zinapofanya kazi kwenye makazi ya Vyuo Vikuu wako katika machafuko makubwa. Hata wakati wa kipindi cha shughuli nyingi sana/pilika pilika ya kesi mahakamani, nilihamasisha msaada toka vyombo vya habari, wataalamu wa kuendesha uchumi, na wana sheria juu ya msingi wa nguvu za falsafa ya Umoja (Unification Thought) unarusha wavu kwa kufunika maelfu ya samaki na unaacha kamba iende, na muda unapofika unaikunja na slingi (winchi). Kamba ambayo unavutia ni falsafa ya Shirika la Umoja. Samaki zote zinavutwa ndani kwa kamba. Lengo, kwa kweli, ni kurudisha samaki zote kwa Mungu. Hiki ni kipindi cha kutoa wavu, hivyo tarehe 1 March 1983, amri ilitolewa Merikani kwa uhamasishaji kamilifu. Ile ilikuwa mwanzo wa kipindi cha miaka mitatu ya malezi kabla ya kuingia nchi ya Kanaani. Miaka hiyo mitatu iko sawa sawa na siku tatu huko Misri wakati watu wa Israeli waliruhusiwa na pharaoh kwenda jangwani kwa sababu ya kumtolea Yahwe sadaka. Wakati wa kipindi hicho cha miaka mitatu, mngefanya kazi kwa njia ya bidii nyingi na nguvu sana. Na vile kama jinsi watu wa Israel walikuwa wanatafuta kudhihirisha utii wao kwa Mungu kwa mmuda wa siku tatu, lazima muishi kipindi chenu miaka mitatu kwa kujitoa mhanga na kupenda. Jangwani, watu 600,000 wa kizazi cha kwanza walikufa, baada ya kushindwa na shetani, lakini kizazi cha pili kiliingia Kanaani. Leo huko Merikani na Japani, kizazi cha kwanza walipinga Shirika la Umoja, lakini kizazi cha pili wanaweza kutotupinga. Tutaelimisha kizazi cha pili.

Sasa tuko katika kipindi cha miaka mitatu jangwani. Ingawa mazingira yetu ni ya uhasama kiwango cha sisi wenyewe kuuana, yatupasa kupenda taifa letu, yatupasa kupenda nchi yetu ya kuzaliwa yatupasa kushinda uhasama wote. Lazima tuwe na juhudi ya roho pia dhana ya kufanya vile. Ile nido kusudi la kipindi cha miaka mitatu. Bila kufundishwa kwao kwa njia ya taabu jangwani, watu wa Israel wasingekuwa na uwezo wo wote wa kushinda na makabila saba ya Kanaani. Vile vile, ila tumefundishwa, hatuta kuwa na uwezo wa kushinda communism. Sisi wana chama wa Shirika la Umoja lazima tuvae kofia ya chuma ya roho ya Kimbingu jangwani ili kushinda uovu. Yatupasa kupata kuwa maaskari ambao wanaweza kupambana na ubaya katika miaka hii mitatu. Kwa hiyo, mahali pote mnakuwa duniani, sikuzote tweka bendera ya ushindi masaa 24 kwa siku. Izungushe katika kila mji, kila mji mkubwa, kila jimbo, kila kijiji, na kila nyumba. Sharti muwe washindi.Lazima mkamilishe kazi yenu kulingana na kusudi la Mungu. Kama sivyo, hatuwezi kutimiza kipito hiki cha maongozi tunachokitembelea ambacho kulingana na kile cha wana Israeli. Lazima mtangazie wazi dunia nzima kwamba Shirika la Umoja liko njiani kwenda nchi ya Kanaani, na kwamba mimi, kiongozi wa Shirika la Umoja, niko katika nafasi ya Musa leo. Katika miaka hiii mitatu, yatupasa kushinda upinzani wote na kujitoa mhanga kabisa kwa Mungu na dunia. Bado hatuna taifa, na tena bado hatuna na mazingira salama(thabiti) kwa familia wabarikiwa, ijapokuwa kuna mataifa na familia nyingi duniani. Kwa hiyo, yatupasa kuaminisha kila kitu kwa nia ya Mungu, na lazima tumsikilize kwa nguvu. Inatubidi kutoa kila kitu kwa ajili ya Mungu na nia yake, na kwa ajili ya kupenda walimwengu wote. Kwa njia ya utumishi yakinifu, yatupasa kupata kuwa moja, kwa kutupilia mbali utii kwa taifa, na kwenda mbele kuelekea Jericho. Hiki ni kile kinacho maanishwa na kipindi cha miaka mitatu.

KUKARIBI KULIPUKA KWA ROHO

Hivyo msiingiwe kamwe na shaka. Wekea kila kitu. Kama una nguvu yo yote, itumie yote. Lazima muwe tayari kutolea maisha yenu upendo wa Mungu. Lazima mjimwage wenyewe, kwa uhakika wa kwamba roho ya upendo huishi daima(ni ya milele). Kila mmoja wetu yampasa kuelewa kwamba tunasimama mapana ya nywele mbali na sehemu ya mwisho wa safari ya maongozi ya Mungu. Katika hali hii, lazima kamwe tusishindwe. Kushindwa kunaweza kuwa na sikitiko. Washiriki wa Shirika la Umoja wa Mashariki na Magharibi lazima wawake na kulipuka pamoja kwa roho duniani kote. Mlipuko wa roho kama huo utatimiza ufufuo wa dunia. Hata Mungu mwenyewe atafufuka kwa sababu roho yake itawekwa huru.

Sisi ni kama maaskari wanatembea mbele kutimiza ukombozi kwa njia ya malipizi. Lazima tuelewe jambo hili vizuri. Tena tuna lengo la kuunganisha dini za dunia. Mwaka huu tunadhamini mazungumzo ya Mungu ya tatu ya mwaka. Yunawaonyesha njia vijana viongozi wa kesho wa dini zote kwa kwenda kwa umoja. Shirika la Umoja ni Shirika timilifu; ni lile la ushirikiano la dini zote na madhehebu yote. Tena ni Shirika lisilojali tofauti za jadi, jinsi tunavyoweza kuona katika ndoa zetu. Juu ya hayo, Shirika la Umoja ni la ushirikiano wa kuadilisha. Kwa sababu ya shughuli kama hizo, wenye akili wengi wanagudnua kwamba Reverend Moon ni mtu peke yake anayefikiri na kutenda na kiwango cha dunia nzila. Watu wengi wamekuja kutambua kwamba ni Reverend Moon peke yake anaweza kutendea kazi matatizo yote ya dunia. Kama tunaweza kukamilisha kazi zetu katika miaka mitatu hii, na kujenga msingi wa ushindi ambao Mungu anaweza kusaidia, hapo vyombo vya utangazaji wa habari watageuza njia yao ya kuandika juu yetu. Ile ni imani yangu. Kama ile ni hali halisi, kipindi cha udhalimu ambacho kinahitaji ukombozi kwa njia ya malipizi(kitageuka hewa) kitapotea, na popote tutaenda, tutapokelewa kwa vifijo vikubwa vitakavyofikia njia yote mpaka Mbinguni, juu ya msingi wa familia. Dhumuni la kazi yetu ni kufanyiza dunia ya umoja, dunia ambayo ina utawala mmoja, nchi moja, utamaduni mmoja, vile ilivyoandikwa kwenye "Ahadi Yangu". Ni ukoo mmoja chini ya fungu lile moja la Wazazi wa Kweli. Tunapata kuwa warithi wa utamaduni huo, kwa kutimiza "Ahadi Yangu".

Tunaenda kukamilisha maneno "mpende adui yako" ndani ya Biblia. Wakristo waliamini kwamba adui wa mtu ni mtu mmoja tu; lakini ile sio kweli kabisa. Shirikia la Umoja linafundisha kwamba adui wa mtu anaweza kuwa taifa moja hata dunia, ambayo hapo mngehitaji kupenda. Mataifa adui wetu wanapata kuwa mahali pa kwanza kwa Ufalme wa Mbinguni wetu. Ila ufalme wetu unaanza toka ndani ya taifa adui, basi Ufalme wa Mbinguni hauwezi kalwe kutimizwa. Kama tutajenga utamaduni wetu kwa njia hii, basi siku zote za mbele hakutainuka fundisho kubwa zaidi. Hii itakuwa fundisho timilifu. Mataifa makuu adui manne yapaswa kuanza Ufalme wa Mbinguni toka kwa utamaduni wa ki-Mbingu wa ushindi huu, kwa kutunga msingi wa upendo dunia nzima. Kama ile itafaulu, hapo Ufalme wa Mbinguni duniani unaweza kuanza. Kwa sababu hiyo, toka sasa katika kipindi cha miaka mitatu ambamo msingi kamilifu wa malipizi unatakiwa kuwekwa. Ila tunakuwa washindi katika miaka mitatu. Tunafuatia ukombozi kwa malipizi, na tunajaribu kukomboa nini? Ukamilifu wa viwango vingi. Ukamilifu wa Adam peke yake ni msingi wa ukamilifu wa familia, ukoo, taifa, na dunia. Baada ya mimi kulipia malipizi yote yanayohitajika kwa kutwaa ushindi toka kwa Shetani juu ya kiwango kipana zaidi, basi nyie, pamoja na walimwengu wote, lazima tena mpate ushindi katika njia mliowekwa mahali maalum. Ile ni dhumuni la shughuli ya Home Church. Kwa njia yake, mtakuwa na uwezo wa kudai sehemu ya nchi iliyokombolewa ya Kanaani kama miliki yenu binafsi.

Kanaani ya leo iko wapi? Ni dunia nzima. Tunakamilisha tayari masharti kwa ushindi/kufaulu kwa maongozi ya Mungu juu ya dunia hii; kupanuka kwa shuguli za Home Church, inapitilia mbali uraia na ideologia. Tunafanya kazi hata katika nchi za kicommunisti. Kwa kupitia kazi za Home Church, tunakomboa Kanaani, na "tunarithi" sehemu ya dunia kwa kudai itibari/heshima kwa kuweza kukomboa kikamilifu ujirani mmoja. Kama anguko la binadamu halikutokea, kila mtu angeweza kupewa haki ya kuwa mmlikaji wa ulimwengu. Home Church yenu itakuwa kitu chenye masharti ambacho kwacho mnaweza kumiliki ulimwengu -vitu vyote, watu wote, wazazi, na Mungu-kwa kufanyiza msingi wa upendo. Kwa hiyo, bila Home Church hamwezi kufanyiza msingi wa kupata kuwa mmoja na Wazazi wa Kweli pia na Mungu. Hamwezi kwenda Ufalme wa Mbinguni bila kufaulu katika Home Church yenu.

MALIPIZI TIMILIFU NA HOME CHURCH

Maishani mwangu nilikamilisha malipizi timilifu na kujenga msingi wa ushindi. Juu ya msingi huu, nilitangaza kuanzishwa kwa shughuli za Home Church. Hii ndio habari nzuri zaidi iwezekanayo kwa walimwengu. Toka Home Church, Ufalme wa Mbinguni duniani, kuwekwa huru kwa Mungu, taifa timilifu, na nia ya kweli yote itatimilizwa. Tunarithi Home Church kuwa kama maisha yetu ya siku zote. Mungu amewapeni kitu cha thamani kama hicho, lakini hamtaki kwenda kwenye maeneo yenu ya Home Church. Kuna watu ambao hata hawana maeneo. Ila mna eneo lenu binafsi la Home Church, ambalo ni kabila lenu la aina ya Kaini, hamuwezi kamwe kukomboa kabila lenu la aina ya Abeli. Kabla ya kuweza kukomboa familia yenu ya aina ya Abeli, lazima mkomboe Kaini kwanza. Hakuna mtu ambaye alielewa jambo hili hadi sasa. Ni muhimu kumpenda adui yako. Kwa sababu gani Mungu alifanya juhudi kwa kutufundisha kwamba kumpenda adui yetu ni muhimu? Shetani anamwambia Mungu,"Ili wewe uwe Mungu, sharti dumisha upeo wa nia, upendo wa milele." Mungu anajibu, "Ndio, ile ni kweli." Halafu shetani anasema, "Mungu, pale uliponifanya mimi kuwa malaika mkuu, eti ulifanya hivyo ili kunipenda kwa muda, au kunipenda daima?" Na Mugnu anasema, "Daima." Kama Mungu angependa kwa muda tu, hapo yeye angekuwa kama Shetani. Vile vile, kama mtu mmoja hana upeo na kupenda daima, yeye hawezi kuonyesha ukii wa Mungu kwa Shetani. Ili Mungu awe Mungu, lazima ampende Shetani haidhuru kwa kadiri gani Shetani anampinga.

Shetani anasema,"Nilianguka na nilipata kuwa mwovu, lakini nyie ambao mko wema hamuwezi kamwe kubadilika, na hamuwezi kamwe kufanya mambo ambayo mimi nayafanya. Nafurahia kushambulia na kupigana, lakini wewe unachukia kupigana. Mungu hawezi kwa nguvu kuzuia shambulio la Shetani. Kwa nini? Mungu hawezi kuvunja nguvu za Shetani hivi hivi. Lazima ampende bila kubadilika badilika ili mwisho wake, Shetani atapata kusema, "Lo! Kwa kweli wewe ndiye Mungu. Najisalimisha kwako." Haidhuru mateso kiasi gani uliwahi kupata, lazima umpende malaika mkuu hadi nia ya Mbingu imefanyizwa kabisa duniani humu. Mikono ya Mungu imefungwa kwa haja ile. Jinsi unavyokwenda njia yako ya Ufalme wa Mbinguni, Shetani atakupima. Vile hata Mungu lazima ampende Shetani na kumuacha Shetani anajisalimisha kwake; vile watoto wa Mungu lazima wampende malaika mkuu kama wanataka kwenda ufalme wa Mbinguni. Ungechukua upendo kiasi gani? Ingwa wewe unadhulumiwa na wote wa dunia hii, ambayo ni ulimwengu wa adui, lazima umpene mtenda mabaya kwa moyo wote. Lile ni sharti, mnatakiwa kukamilisha. Mungu ni yule anayehuskia zaidi juu ya sharti lile, basi wale watu ambao wanajitahidi kuwa watoto wa Mungu na wao tena wangehusika juu yake; Upeo huu wa kupenda ungeweza kuonekana mwepesi, lakini ule ni mstari wa mpaka kweli kati ya Mungu na shetani. Hakuna aliye elewa hii kabisa hadi sasa. Ili kuvuka mipaka hii, Mungu hawezi hata kumuangalia adui wake kama adui, na lazima asilipize kisasi.

Neno letu la mwisho ni kupenda adui zetu. Yesu alipoomba kwa ajili ya wale watu ambao walikuwa wanaumwa, ilikuwa ushindi mkubwa zaidi. Kama aliwachukia maadui zake wakati alikuwa akikaribia kufa, basi jambo la Mungu lisingefaulu. Lakini hapo Yesu alishinda matatizo yake kwa njia ya upendo, Shetani alianza kujisalimisha, na Yesu alipewa sifa za mtoto makamilifu wa Mungu. Lazima mfikie mahali ambapo mnakuwa na uwezo wa kusema, "Shetani, je hukubali kwamba mimi ni mtoto wa Mungu?" na kumpata Shetani anakiri, "ndio, ile ni kweli." Lazima muwe na uwezo wa kusema kwa kujiamini," ninafuata mwongozo wa Mungu, kwa kupanua ulimwengu wa upendo wake toka kiwango cha mtu peke yake, kwa kupitia familia, jamii na taifa, hadi kiwango cha dunia nzima. Wewe huna katazo lolote hapo? Sawa, Shetani?" Na Shetani lazima aseme, "Yanipasa kukukubalia kwa sababu ya kanuni." Hii ni jinsi alivyoendeleza maongozi yake, chini ya maongozi yake, chini ya uongozi wa Ukristo. Ilikuwa njia ya kujitoa mhanga na kuteswa bure na, kwa kupitia historia yake katili, ya kiuaji, Ukristo ulikuwa Shirika la kusambaza upendo wa Mungu kwa kiwango cha familia, kiwango cha jamii, kiwango cha taifa, njia yote hadi kiwango cha dunia nzima. Kwa kupitia upendo wa Kikristo, ambao unapenda adui, mataifa maadui yanaweza kushindwa; kaini ameshindwa kabisa. Kwa kufuata njia hii, Shirika la Umoja limetawanywa duniani kote.

UPENDO NA WATU WA JAPAN

Kwa mtazamo wa kidunia, watu wa Japan wanapaswa kuwa maadui wangu. Walishinda Korea na kuwafanyia watu wa Korea mambo mabaya mengi, kwa kuwa maelfu tangu 1905 hadi 1945. Hata hivyo, ninapenda watu wa Japan. Japan alipojisalimisha kati ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, niliwapenda maadui wangu walioshindwa. Hii ndio sababu washirika wa Japan sasa wananifuata kwa kuhatarisha laisha yao; hii ni kwa kulingana na kanuni ya uhusiano kati ya chanzo na tukio. Ni kwa sababu niliweka msingi wa roho kwa kupenda taifa qdui, Japa, kwa roho ya Mungu, kwa kuzidi fahari ya taifa langu. Maaskari polisi wa Japan ambao walinipiga karibu na kuniua wangeuana baadaye kama nliwatatanisha. Lakini niwasamehe na niliwaaga vizuri kwa kuwarudisha Japan na mizigo yao. Aidha, inakuwa kitu kizuri kwamba washiriki wa Japan sasa wanamwaga machozi, jasho, na damu kwa kuokoa U.S., ambaye zamani alikuwa adui wa Japan. Kwa njia hii, Shetani anakuwa analazimika kuacha jimbo lake na kiwango cha dunia nzima. Vijana washiriki wa Japani sasa wanafanya kazi kwa nguvu kwa kuhatirisha maisha yao kwa ajili ya U.S., nchi adui tangu miaka 37 tu, kwa ajili ya kuiokoa na kuiunganisha na Mbingu. Hili ni tukio la kustaajabisha, kitu kingine ambacho kamwe hakijawahi kuonekana katika historia. Kwa sababu gani washiriki wajapani wanafanya hivi? Hawafanyi kazi U.S. peke yake, lakini ni kwa dunia. Basi watu wa Amerika wasiishi kwa kulingana na desturi ya uchoyo. Nilimwambia kiongozi Mmerikani mmoja wa Kanisa la Umoja juzi juzi kwamba washiriki wote wamerikani wana njia yao ya kawaida ya kuanza. Kwa tabia kala hiyo, hamwezi kukamilisha shughuli ya kadiri ya dunia. Mngeelewa kwamba mnaweza kufanyiza utamaduni wa upendo wa dunia nzima mara tu mshindapo matamanio yenu binafsi. Mngefanya kazi ngumu kuliko waumini wa Japani, maadui wenu wa zamani. Ni aibu kwenu kwamba maadui zenu wa zamani wanawatendea kazi zaidi msishindwe kwa upendo na wajapani. Waumini wazungu, sana sana wajerumani, ambao wamebarikiwa na waumini wamerikani wote wangekuja Merikani, kwa sababu america ni mlango kwa dunia. America sio taifa kwa ajili yake; inawakilisha dunia ya kidemokrasia. Kwa hiyo, mimi sasa nahamasiha waumini sehemu zote za dunia kwa ajili ya America ili kufanya nchi hii kuwa kiini cha utamaduni mpya chini ya Mungu pia kiini cha Shirika la Umoja siku zijazo;

Hata kama Japan ilipata kuwajangwa kiroho, mngezidi kuishi kama U.S. inaishi. Kwa hiyo, mngejifunga wanyewe kwa kuendeleza kiroho America. Nilileta hapa baadhi ya mila na desturi ya Korea juu ya msingi wa utakaso na (wema) adilifu, ili kuokoa nchi hii. Nilikuwa nafanya hivyo kwa kulingana na kanuni, na kwa hiyo kuendeleza Shirika la Umoja. Taifa Eva Japan, inabidi iungane na taifa Adam, Korea Kusini, baada ya kufundisha mataifa Kaini na Abeli utamaduni wa Mbinguni. Kwa maneno mengine, lazima muwafundishe wajerumani na wamerikani, mmoja mmoja. Hii ni kulingana na kanuni. Kalma mtashindwa, hamwezi taifa Eva. Kwa mtazamo huu, ulinzi wa Korea ni suala la hatari kwa mlindo wa Japan. Hii ni neno la mwisho kwa mtazamo wa maongozi. Kwa ajili ya kuunganisha Japan na Amerika-kwa vyote mwili na roho- wazo moja ni kujenga shimo refu la kupitia chini ya bahari kati yao. Tumeingia sasa kipindi kimoja muhimu cha ajabu sana. Kile ambacho nina kishughulikia sasa ni kazi ya mwisho kihistoria, hahali pa mwihso mwa historia. Ninakusanya na kuunganisha sasa mataifa makuu manne katika maongozi, kwa kutoa sadaka umoja wao kwa Mungu kama sharti ya malipizi kubwa mno kupitia kiasi kwa kukomboa dunia. Umoja kama huo unapokamilika, Ufalme wa Mbinguni utaanza, basi hii ni mwanzo wa wakati huo huo ni mwisho wa maongozi ya Mugnu. Kama tutaendelea mwendo kama huo kuelekea umoja kwa miaka mitatu ijayo, hakuna mtu atakaepinga kazi yetu.

Huko Amerika Kusini, watu tayari wanasema, "Karibu, Reverend Moon." Ni vile vile huko Africa na Asia, pamoja na kati ya umati wa wajapan na wa china katika United States. Kama vikundi vya wachache kama hizi vitaungana kabisa, kundi la wingi litapata kuwa kundi la wachache. Hapo chuki yao ya miaka mingi dhidi ya wamerikani weupe lazima itumike sio kwa kulipiza kisasi lakini igeuzwe kuwa upendo kwa kuokoa "adui". Ile ni shauri kwa msingi wa upendo wa Mungu. Kama mtafanya kazi kwa nia kama hiyo, mnaweza kufanyiza sharti ya malipizi kamilifu. Kufanyiza sharti la malipizi kamilifu maana yake ni ukombozi timilifu. Basi, ukombozi timilifu unaongoza wapi? Unaongoza kwa ukamilifu timilifu.

MATAIFA MANNE KATIKA MAONGOZI

Kama tutaweza kukomboa mataifa makuu manne katika maongozi, tunaweza kumtolea Mungu viasili vya msingi ambavyo vilikuwa vya Shetani. Mataifa manne haya katika maongozi wanaleta pamoja viasili hivi vyote vya msingi. Korea ina nini? Roho na johari la wazo. Japan ni uzuri, United States in anguvu na Ujerumani ina ustadi na ubingwa. Mataifa manne haya kwa pamoja yaina vitu vyote vinavyoweza kuleta umoja kote kote duniani. Kuanzia na kiwango cha mtu peke yake, kwenda kupitia familia, ukoo, jamii, na kiwango cha taifa, tumifa sasa na kiwango cha kufanyiza masharti ya malipizi na kiwango cha dunia. Mataifa makuu manne ambayo zamani yalikuwa maadui sasa yanapata kuwa yamefungana chini ya mila na desturi ya Mbinguni. Kwa hiyo, Ufalme wa Mbinguni duniani hauko mbali. Uko karibu sana. Mnapong'amua hili, mngeng'oa vizuizi vyote, kwa kufanya kazi kwa moyo wa shukrani hata kwa kuhatarisha maisha yenu. Kwa hivyo, nyie waumini ambao mnarudi Japan mngejaribu kufanya kazi mara tatu zaidi kuliko (waumini) wamerikani. Hata ukiondoka barabarani vile kama mti ulioanguka, lalamika. Mngejaribu kufanya kazi mkiwa na roho isiyochoka kwa bidii kwa miaka mitatu hii, hata kwa kupata mlo mmoja kwa siku. Hii ni kikomo cha historia. Ninawaulizeni kushuhudia kwa haraka sana nchini kote kwa miaka mitatu. Kwa kuimarisha ushuhuda, ninafikiri kutumia utangazaji kwa radio. Kama tena tutatumia teknologia ya satellite, tungeweza kushuhudia kwa sehemu iliyokubwa zaidi ya walimwengu kwa juma moja. Miaka mitatu kweli haihitajiki kwa kukamilisha kazi ya Shirika la Umoja. Inatubidi kujenga Shirika moja la nguvu kabisa kiasi cha kuifanya communism kidunia haiwezi kutolitambua. Hii sio hadithi tu; ni jambo la kweli. Kama tunaweza kujenga Shirika kama hili, mnaweza kuhamasisha na kuweka huru vizazi 70 au hata 120 vya mababu zenu. Watu katika ulimwengu wa kiroho wana hamu kuisaidia dunia. Kama mtahamasisha mababu zenu, mnaweza kuvuta wafuasi 70 na halafu wafuasi 120 chini ya uongozi wa ukoo wenu. Hili ni tukio kubwa. Sababu ya nyie kujiunga na Shirika la Umoja sio kwamba mnayo stahiki kubwa kiasi hicho au imani ya nguvu; Mliweza kujiunga kwa sababu ya mababu zenu, sadaka ya maelfu ya vizazi vya mababu zenu, na utumishi na wema wao kwa kusudi la Mungu. Kwa hiyo, mtapata kuwa wa nani kama hamnifuati na kufanya kazi kwa ajili ya taifa na dunia? Mababu zenu watakasirika na nyie na kuwasuta kwa kutowajibika mtakapokwenda katika dunia. Kiroho, hamtakuwa na mahali pa kwenda. Lakini, kama mnapokamilisha utume wenu na baadaye kwenda duniani kiroho, mtapokelewa hapa sio na msingi wa ukubwa wenu; mlihamasishwa na mtirirko wa roho.

Nilikuja hapa kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kihistoria, na Mungu aliandaa mazingira kwa ajili yangu. Ndivyo ilivyo katika kanuni za uumbaji kwamba mazingira yanaandaliwa; kila kitu duniani lazima kipitie kipindi cha ukuzi. Kwa hiyo, dunia kiroho iliwahamasisha mlipo. Basi, msingeishi maissha mepesi. Mngekataa njia ya kuwaza ya kawaida na kukaza akili yenu juu ya wema; fanya kazi kwa moyo wenu wote, kwa kukumbuka upeo wa roho ambao mmeupokea toka kwangu leo. Imewapasa kufanya kazi kuanzia sasa kwa njia tofauti na vile mlivyo zoea. Kwa mfano, imewapasa kumfanya mkewe kufanya kazi kwenye manowari kubwa na imewapasa kutabaruku watoto wenu kwa kusudi hiyo pia. Kweli, hamwezi kupenda watoto wenu bila kwanza kupenda watu wengine. Vinginevyo, Shetani anaweza kuwasuta. Imewapasa kujitahidi kupata sahihi ya Shetani, kwa kujalisha kwamba mnapenda watu wote waliopo chini ya utawala wake. Halafu mnapata kustahili kurudi nyumbani kwenu na kwa uhuru penda watoto wenu, familia yenu, ukoo wenu na taifa lenu. Hii ndio kanuni ambayo mimi mwenyewe nilikuwa nayo na nikaishi. Siku kazana juu ya kuwajali watoto wangu. Siku walea watoto wangu peke yangu, hata wakati nilikuwa naishi East Garden. Ijapokuwa, ni nani alimlea Adam? Ni malaika mkuu. Mungu, Baba wa Adam na Eva, hakuwalea yeye mwenyewe mara moja. Kwa hiyo, ni nani angetakiwa kulea watoto wangu? Familia wabarikiwe 36, ambao wanasimama na nafasi ya malaika mkuu. Njia ya mazoea, ya kikanuni kama hiyo kwa kulea haijafanyizwa ndani ya Kanisa la Umoja. Kama kunakuwepo na washiriki miongoni mwa familia wabarikiwe 36 ambao wanalalamika juu ya watoto wangu, ni kweli tatizo. Lazima niyatatue malalamiko hayo.

Lazima mpende Kaini na kiwango cha familia; hata mnaweza kumpenda Kaini na kiwango cha mtu peke yake. Lakini mnahitaji kwanza kumpenda Kaini na kiwango cha jamii pia na kiwango cha taifa. Hii ni kanuni ya ukombozi. Ka hivyo, furaha ya mtu mmoja inapaswa kutolewa sadaka kwa ajili ya kukomboa dunia. Kwa kusudi hii, nilijifunga mwenyewe na hata uthabiti/mali ya Shirika la Umoja kwa kujenga United States. Baada nyie kufanyiza sharti la malipizi la upendo na sadaka na kiwango cha dunia nzima, basi mnaweza kurudi nyumbani na kuwapa watoto wenu upendo mkubwa kuliko ule mliompa Kaini. Familia ya Abeli takatifu na familia ya Kaini hawana budi kuungana na kiwango mlalo. Imewapasa nyie kupenda watu wa Japan pia watoto wangu, na baada ya wote watu wa Japan na watoto wangu kuwasifu nyie mnaweza kupenda watoto wenu nyie wenyewe. Hii ndio kanuni kama watoto wangu walipitia wakati wa taabu kwa sababu ya kutojaliwa na familia wabarikiwe 36, mimi siku nung'unika. Ile ilikuwa sharti la malipizi. Siwezi kupewa familia wabarikiwa 36. Kwa tumaini kwamba watakuja kuitumikia familia yangu jinsi inavyotakiwa, nilikuwa nawakumbatia siku zote kwa upendo. Inabidi msiwe majuzi kwao, kwa sababu Shetani anajaribu kushambulia kwa njia ile.

Kama mnaweza kuzidia kiwango cha kitaifa chza roho na kuoonyesha upendo ambao shetani hana budi kujisalimisha basi kila kitu kitakamilika. Nilimuuliza mwanachuo maarufu wa katiba wa U.S kufanya mwandiko wa upesi wa katiba kwa Ufalme wa Mbinguni. Muda kama huo unakaribia sasa. Kwa sababu tumekuwa karibu kiasi hicho kwa utimilifu wa maongozi ya Mungu, imewapasa nyie kuelewa kwa kiwango gani nafasi yenu iko muhimu na ya thamani; huu ni wakati imewapasa kurekebisha njia yenu ya maisha. Kati ya maisha yetu tangu sasa hivi, hatuna budi kurudia makosa yetu ya zamani, walakini imetupasa kulemeza/kukaza mbele kwa kufanikiwa kukamilisha kusudi la Mungu. Ile ni tumaini langu. Sasa acheni tuombe, kwa kuinua roho zetu Mbinguni.

 

 

Mpendwa, Baba mpenzi Mbinguni,

Kwa kupitia enzi zote za historia, wewe (uliwezesha) uliweka dini nyingi kwa ajili ya kuweka huru roho yako iliyokuwa inahuzunika. Kwa kutoa sadaka viongozi waaminifu wengi, ulikuwa unaendelea mbele kuelekea ushindi wa mwisho wa upendo wako. (Ninapotazamia) Ninapofikiri habari za historia hii na kadiri ya malipizi yaliyolipiwa na watu wangapi waliteseka, ninasikitika sana Mbingu. Wewe uliandaa vitu/mambo ili tuweze wakati mpya. Liache Shirika la Umoja hili lifanikiwe duniani. Uliwezesha, Baba wa Mbinguni, kwa Reverend Moon kuja duniani na kutufunulia leo maneno haya ya maana. Tuache tuelewe ujumbe huu. Tuna toa shukurani kwako, na kwa dunia hii kubwa, na tunaionyesha kwa kunyanyua mikono yetu yote (juu). Sisi tuliahidi na tunaahidi mara nyingine tena kutenda mbele kwa kuhatirisha maisha yetu juu ya uwanja wa mapigano yoyote kwa sababu ya nia yako. Tunakuomba kwa moyo, Baba kupokea/kukubali nia yetu hii kwa furaha.

Hapa, wawakilishi wa mataifa mbalimbali wamekusanyika, kwa kuzidi uraia wao. Tafadhali elekeza pia tawala/ongoza wale ambao wako hapa umetufanyiza kuungana chini ya upendo wako mtakatifu, na umewayeyusha kwa pamoja maadui asilia pia ulikuwa unaendeleza ulimwengu wa upendo. Sasa tunaelewa mambo haya yote. Basi tulikuahidi kutotenda tendo lolote ambalo linapinga desturi ya nia yako, haidhuru katika jambo hili la mambo ya aina gani tunajikuta. Na tafadhali endelea kututia moyo/kutushawishi ili tuweze kupata kuwa watu ambao wana jikaza ijapokuwa udhalimu wowote. Tunaahidi kwenda mbele kwa kufaa kutumia muda wetu unaobaki hadi tutaingia ndani ya dunia timilifu ya nia yako. Kwa moyo, nakuomba utuelekeze upande wa majina ya nia yako ili tuweze kulifuata kwa uhakika. Ninaomba haya yote kwa moyo, na kutoa sala hii katika jina la Wazazi wa Kweli. Amina.